Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa akiongea wakati wa Baraza la madiwani la kupitisha rasimu ya bajeti ya mwaka 2023/2024


Na Fredy Mgunda, Iringa.


HALMASHAURI ya Wilaya ya Iringa imepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 wa kiasi Cha shilingi bilion 60.24 ikiwa na ongezeko tofauti na bajeti ya mwaka 2022/2023.

Akizungumza kwenye Baraza la madiwani, mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Stephen Mhapa alisema kuwa wamepitisha rasmi ya bajeti ya shilingi bilioni 60,245,770,237 imepanda Kwa asilimia 2 kutoka asilimia 15 hadi asilimia 17 katika mwaka wa fedha wa 2023/2024. 

Mhapa alisema kuwa Halmashauri imepanga kukusanya na kutumia shilingi 6,592,471,590 Kwa mapato ya ndani ambazo zinajumuisha ukomo wa bajeti kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi ngazi ya chini.

Mhapa ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa Dk Samia Suluhu Hassan, akisema imeendelea kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Kwa upande wake afisa mipango wa Halmashauri Exavery Luyangaza alisema kuwa mapato ya ndani ya Halmashauri yameongezeka kutoka shilingi 4,269,100,000 mwaka 2022/2023 hadi shilingi 4,995,665,000 sawa na asilimia 17 ya kiasi kilichoongezeka na kusaidia utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri.

Luyangaza alisema kuwa rasimu ya bajeti hiyo imekidhi matakwa ya mipango ya maendeleo ya Halmashauri hiyo na kusaidia kukuza uchumi kwa Wananchi.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa walipongeza bajeti hiyo kuwa itakidhi haja ya kutatua changamoto za Wananchi na kuwaletea maendeleo.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: