Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) na Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe, Dk Festo Dugange amesema hospitali mpya za wilaya 135 zimejengwa nchi nzima katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
Amasema hayo Februri 5, 2023 mkoani Njombe, wakati akieleza utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika maadhimisho ya miaka 46 kuzaliwa kwa CCM kimkoa.
Amesema Rais Samia ameimarisha utoaji wa huduma za afya nchini, ambapo amewezesha ujenzi wa zahanati na ukamilishaji wa maboma ya zahanati zaidi ya 1,000 vituo vya afya zaidi ya 390 nchi nzima.
Amesema Rais Samia amewezesha ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, ambayo inatoa huduma za mionzi na huduma nyingine ambazo ziliwalazimu wananchi kuzifuata mikoa mingine.
Amesema Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa 10 ya awali iliyopata shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya maalum ya wasichana kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita inayoendelea kujengwa mkoani hapo.
Post A Comment: