Na Joel Maduka Geita. 

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabau ya Geita Gold Mine (GGML) imetoa mbegu za Alizeti  kilogram 23,000  zenye thamani ya milioni 108 ambazo zitawanufaisha wakulima 3701.



Akizungumza  kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mgodi wa GGML,wakati wa kukabidhi mbegu za Alizeti   kwa wakulima wa Halmashauri Mbili ya Mji wa  Geita na Halmashauri ya Wilaya ya Geita zoezi ambalo limefanyika  kwenye kijiji cha Kasota Kata ya Bugulula ,Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii GGML,Gilbert Mworia,amesema wamefanya hivyo kwa wakulima kwa lengo la kuongeza mbinu za kujiajiri kwa wananchi pamoja na kupunguza uhaba wa mafuta ya kula.



"Tumekuwa tukiwasaidia wakulima wa alizeti na mpunga kwa kuwapatia trekta na kulima mashamba yao.Lengo ni kuwa na wakulima wanaojitegemea na wenye miradi endelevu na watakaojitegemea hata baada ya GGML kumaliza shughuli za uwekezaji katika Wilaya ya Geita"Gilbert Mworia meneja mwandamizi wa mahusiano ya Jamii GGML. 



Mkuu wa Wilaya ya Geita,Cornel Magembe ,amesema kilio cha alizeti kimekuwa na tija kwa kuwainua wakulima wengi Zaidi kutokana na uwitaji wa mafuta.



"Kilimo cha Alizeti kimekuwa na Tija kubwa kwa wakulima na wengi sasa wameendelea kufanikiwa kupitia kilimo hiki Niwasisitize wakulima waliopatiwa mbegu limeni kilimo cha Alizeti ni bora sana kwani kinafaida nyingi sanaa"Cornel Magembe Mkuu wa wilaya ya Geita. 



Tangu kurekebisha kwa sheria ya madini mwaka 2017,GGML imetumia zaidi ya Shilingi za kitanzania Bilioni 30 kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii kwa kushirikiana na Halmashauri zilizopo Geita.



Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: