Watendaji kata wametakiwa kufanyia kazi vifaa ambavyo serikali imeendelea kuwapatia kwa kuwasaidi katika utendaji wao wa kazi huku wakitakiwa kusikiliza changamoto za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Naibu wa Waziri Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametoa maelekezo hayo alipokua akigawa pikipiki kwa watendaji wa kata 6 za Halmashauri ya Chalinze.
“Watendaji nawakumbusha kutumia vifaa hivi kuzingatia makusudio ya kutolewa kwake, nendeni mkawasikilize wananchi na kutoa ufumbuzi wa changamoto zao”.Alisema Kikwete
Kadhalika Mh. Kikwete Ametembelea kiwanda cha Uzalishaji wa marumaru cha Keda, na kuwashukuru wawekezaji kwa kutambua mchango wa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Naibu waziri huyo amepokea vifaa tiba kwa ajili ya Vituo Vya Afya Viwili Kata za Kibindu na Msata, Zahanati katika Vijiji 11.
Katika makabidhiano ya vifaa tiba amewahimiza watoa huduma za afya kuvitunza na kuvitumia kwa makusudio yake.
“Kazi kubwa inaelekezwa kituo cha Afya ambapo kazi ya ujenzi wa miundo mbinu inapaswa kuwa kipaumbele”.Alisema
Post A Comment: