Na Denis Chambi, Tanga.

LICHA ya uwepo wa madawati mbalimbali ya kijinsia yaliyoundwa mahususi kwaajili ya wahanga wa matukio ya ukatili kuepeleka malalamiko yao ili kupatiwa msaada wa kisheria jamii , wazazi, walezi na serikali kwa ujumla imeobwa kuongeza kasi ya utoaji elimu kupitia njia mbalimbali hii ikilenga hasa kuunga mkono jitihada zinazofanyika kutokomeza ukatili uliokithiri hasa kwa makundi ya watoto na wanawake. 

Wito huo umetolewa na mkuu wa shule ya Sekondary St. Christina iliyopo jijini Tanga Hilda Kaniki wakati akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwakwe juu ya matokeo ya kidato cha ne kwa mwaka 2022/2023 ambapo amesema licha ya uwepo wa madawati ya kijinsia yaliyoundwa mashuleni kwaajili ya kuripoti taarifa za ukatili wa aina mbalimbali ipo haja ya kuongeza kutoa elimu kwa jamii sambamba na kuwaongezea uelewa wananchi umuhimu wa kutoa taarifa za ukatili pale zinapotokea katika mazingira wanayoishi.

 "Maswala ya ukatili wa kijinsia ni jambo ambalo limeanza kwa muda mrefu ndani ya jamii zetu na ni kubwa hili pengine linaweza kuchangiwa na utandawazi, tunaona serikali imeanzisha madawati ya kijinsia mashuleni kwaajili ya watoto wa kike na hata kwetu lipo ili watoto wakike kuweza kupaza sauti kwenye haya madawati na hatimaye kupata suluhu ya matatizo yao"

 " Utoaji wa elimu kwa watoto wa kike na hata jamii unahitajika sana pia ni jambo la muhimu ili kujua haki zao ni zipi na kujua viashiria vyovyote vya ukatili wa kijinsia dhidi yao, muda mwingine mtu anaweza akawa anapitia ukatili wa kijinsia na asielewe kama anafanyiwa ukatili wa kijinsia akaona ni kitu cha kawaida , inahitajika kuendelea kutoa hamasa na kuongeza uelewa kuhusu ukatili na wale wanaotoa taarifa za ukatili wa kijinsia wapatiwe suluhu mapema ili kurahisisha utoaji haki kabla ya maafa kutokea " alisema Kaniki. 

Akizungumzia matokeoyaliyotangazwa kitaifa hivi karibuni amesema kuwa ufaulu wa shule hiyo umepanda ukulinganuisha na matokeo ya mwaka jana 2021 ambapo mwaka huu wamefanikiwa kufaulisha wanafunzi 59 kwa daraja la kwanza wengine 15 wakipata daraja la pili matokeo ambaya yanachagizwa zaidi na usimamizi mzuri wa uongozi wa shule ambao umejikita katika kuhakikisha unafikia malengo waliyojiwekea ya kuendelea kufanya vizuri kimkoa na Tanzania kiujumla wakizidi kujipanga kiushindani zaidi katika sekta ya elimu.

 "Shule ya St. Christina wanafunzi wetu wamefanya vizuri sana tuimefurahi kwa sababu tupo ndani ya malengo ambayo tulikuwa tumejiwekea kwa mwaka 2022 na kwa matokeo yetu tuliyoyapata tuna ufaulu wa daraja la kwanza wanafunzi 59 na 15 wamepata daraja la pili na ufaulu kwa mwaka huu umepanda ukitofautisha na matokeo ya mwaka 2021, kuna ushindani mkubwa lakini sisi kama taasisi tunasimamia sana kauli mbiu ya shule malengo na maono ya shule na mikakati mbalimbali ambayo shule imejiwekea, kila mdau wa shule hajawahi kulala hii inatusaidia sana tukishirikiana kwa pamoja" alisema Kaniki. 

Wakizungumza mtaaluma wa shule hiyo Viktoria Mashele amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwaleta watoto wao katika maadili mema ambayo yana uhusiano mkubwa na mwenendo mzuri katika upande elimu hasa wakati anapofundishwa na kujifunza masomo mbalimbali kwa nadharia au kwa vitendo huku makamu mkuu wa shule hiyo George Ngoda akiiomba jamii kwa ujuumla kuwa mstari wa mbele kuungana na serikali pamoja na wadau mbalimbali kuibua vitendo vya ukatili wa kijinsia pale vinapotokea sheria iweze kuchukuwa mkondo wake. 

"Ni lazima kuwajengea uwezo watoto wetu kuwa na uthubutu wa kuripoti vitndo vya ukatili wa kijinsia wito kwa wazazi na walezi tuendelee kuwalea watoto wetu katika maadili nakuwashauri kuwaonyesha ni kwa namna gani wanaweza kuepukana na ukatili wa kijinsia ambao uchangia kushuka kwa kiwango chaelimu kwa wanafunzi" alisema Masele 

"Sisi ni walimu, wazazi na walezi kwahiyo tunalo jukumu kubwa sana katika kuhakisha kwamba ndani ya jamii watoto wetu wote wanaishi kwenye mazingira salama bila kuwa na aina yeyote ile ya manyanyaso ndani ya jamii" alisema Ngoda. 
Makamu mkuu wa shule ya Sekondary St. Christina George Ngoda iliyopo jijini Tanga akiwa pamoja na mtaaluma wa shule hiyo Viktoria Mashele  wakati mkuu wa shule Hilda Kaniki  akizungumza na waandishi wa habari  leo February 2,2023 kuhusu matokeo ya kidato cha nne.

Baadhi ya walimu wa shule ya St. Christina wakiwa  kwenye ofisi ya mkuu wa shule hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari .


Baadhi ya wanafunzi wa shule sekondary St.Christina iliyopo jijini Tanga  wakiwa darasani.

Share To:

Post A Comment: