IMG-20230206-WA0149


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Benny Ndomba amesema katika kuelekea kikao kazi Cha 3 Cha Serikali mtandao ambacho kinatarajia kufanyika Jijini Arusha mamlaka hiyo imejipanga kuandaa na kutekeleza sehemu moja ambayo huduma ya Mitandao zote zinakua zinapatika kwa urahisi.

Akizungumza na waandishi wa habari Februaro 6, 2023 Jijini Dodoma Mkurugenzi huyo amesema kuwa Mamlaka hiyo imepanga kuweka mwelekeo wa Serikali katika kuandaa na kutekeleza mikakati madhubuti lengo ikiwa ni kufikia uwezo wa kutumia teknolojia mpya zinazoibuka hasa zile za akili bandia na sarafu za kidijitali na teknolojia za kifedha.


"Mamlaka ya serikali mtandao (eGA), tumapanga kuhakikisha taasisi zote za Umma wakiwemo maafisa Masuhuli ,wajumbe wa Bodi ,wakuu wa vitengo vya TEHAMA maafisa TEHAMA,maafisa Rasilimali watu,Maafisa mipango ,maafisa Mawasiliano,wahasibu pamoja na watumishi wote wa mifumo ya TEHAMA Serikali hao wote washiriki kikao kazi hicho lengo lete ni kufanya mifumo iwe jumuishi!"amesema Ndomba

Kuelekea kikao kazi hicho Mhandisi Ndomba amesema lengo kubwa ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Serikali Mitandao Ili kujadiliana juu ya mafanikio ,changamoto pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya kukuza Serikali mtandao matumizi sahihi na salama ya TEHAMA katika Taasisi za Umma.


Mamlaka ya serikali mtandao eGA inatarajia kupokea wadau elfu moja (1000) kutoka katika mashirika na Taasisi za Umma wakiwemo maafisa Masuhuli ,wajumbe wa Bodi ,wakuu wa vitengo vya TEHAMA maafisa TEHAMA,maafisa Rasilimali watu,Maafisa mipango ,maafisa Mawasiliano,wahasibu pamoja na watumishi wote wa mifumo ya TEHAMA Serikali hao wote wanatarajia kushiriki kikao kazi kitakachofanyika kuanzia February 8-10 Jijini Arusha.
Share To:

Post A Comment: