Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wataalam na viongozi wa wilaya ya Nachingwea umuhimu wa kukamilika barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wataalam na viongozi wa wilaya ya Nachingwea umuhimu wa kukamilika barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Na Fredy Mgunda, Nachingwea
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amemtaka mkandarasi anayejenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka kituo cha Polisi kwenda soko la Voda kujisalimisha Mara moja kituo cha polisi au ofisini kwake.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami,Moyo alisema kuwa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo inayochochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Moyo alimuagiza meneja wa TARURA wilaya ya Nachingwea kuhakikisha mkandarasi huyo anafika ofisi kwake mara moja na kuanza ujenzi wa barabara hiyo ambayo wananchi wamekuwa wanaisubilia kwa muda mrefu sasa.
Alisema kuwa Wananchi wanataka barabara ya lami sio maneno na huu sio wakati wa kuwabembeleza wakandarasi ambao wanachelewesha miradi kwa makusudi.
Moyo alimazia kwa kusema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan anapeleka fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na sio kwa wakandarasi wanaochelewesha miradi ya maendeleo.
Post A Comment: