Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Rutahengerwa ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa jiji la Arusha kuhakikisha vibanda vilivyopo wazi katika soko namba68 Kilombero vinagaiwa kwa wafanyabiashara.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya katika soko la kilombero kwa lengo la kuangalia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa soko hilo.
"Vibanda ambavyo havina watu vinafika zaidi ya 300 katika soko hili sasa hatuwezi kusema soko limejaa wakati watu wameshikilia meza na hawapo sokoni hiyo haikubaliki"Alisema Felician
Mbali na hayo Mkuu huyo wa wilaya amesema changamoto nyingine waliyoiona ni idadi kubwa ya watoto wanaokuwepo katika soko hilo nakuagiza watoto kutokupelekwa sokoni kutokana na kuwepo kwa lugha mbaya za matusi.
Amesema mtoto mdogo ni mwepesi sana wakushika neno linapotamkwa na sokoni kuna kila aina ya watu wanaoishi humu hii itawaathiri Watoto kisaikolojia.
"Lazima Watoto walelewe kwenye maadili yanayotakiwa lakini maisha ya huku sokoni kwa watoto hayana Afya "Alisema Mkuu wa wilaya
Akipokea maelekezo hayo Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Arusha Hargeney Chitukuro amesema wafanyabiashara hao wamekimbia vibanda na wameenda kupanga bidhaa chini wanakodai kuwa kuna wateja jambo ambalo sio kweli.
Amesema wateja Wana desturi ya kufata mahali bidhaa inapatikana lakini kwa kitu wanachofanya hao waliotelekeza vibanda ni nje ya utaratibu na hawata wafumbia macho.
"Mimi pamoja na wahandisi wangu tutagawa meza hizo kama wahusika hawatarudi ndani ya muda mfupi kwani inaonekana utekelezaji unasuasua na sisi tunataka masoko yawe katika upangilio mzuri"Alisema Chitukulu.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Rutahengerwa akimuungisha mfanyabiashara wa mboga za majani kama kutambua harakati za wananchi wake.Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Arusha Hargeney Chitukuro akichagua matunda ya wafanyabiashara waliopanga juu ya meza.Picha ya pamoja na wafanyabiashara.Mkuu wa wilaya akinywa chai kwenye eneo la soko la kilombero namba 68 mara baada ya kumaliza ziara ya kushtukiza .
Post A Comment: