Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa amewatahadharisha watumishi wa Jiji la Arusha kuwa wasiifanye halmashauri hiyo kama shamba la bibi bali waongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato.
Dc Mtahengerwa atoa wito huo wakati wa kikao cha robo ya pili ya mwaka 2022/23 cha Baraza la Madiwani Jiji la Arusha.
Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakifanya jiji hilo kama shamba la bibi hivyo wafahamu kuwa anajua maeneo yote na alishangaa kwanini Jiji la Arusha litenge bajeti ya Sh bilioni 35 kwa mwaka ilhali linauwezo wa kukusanya Sh bilioni 100.
“Simamieni mapato lakini mdhibiti matumizi haiwezekani watu wanashindana kuumiza wananchi nikiangalia magroupu yenu kunawatu wanashindana upigaji,hebu badilikeni uzuri nazijua chocho zote za Arusha fikirieni vitu vikubwa badala ya kufikiria vitu vidogo”
Amesema lazima sasa Jiji liongeze kasi ya ukusanyaji mapato na kufikia sh,milioni 100 au zaidi lakini pia akatoa salamu kwa wanasiasa kutoa elimu kwa wafanyabiashara kufanya biashara zao katika maeneo yaliyopangiwa badala ya kuharibu taswira nzuri ya Jiji la Arusha kwa baadhi yao kuuza bidhaa zao kwenye maeneo wasiyotakiwa
Post A Comment: