Na Fredy Mgunda, Iringa.
BARAZA la manispaa ya Iringa limewaomba madereva wa daladala manispaa ya Iringa kusitisha mgomo dhidi ya madereva bajaji ambao wamekuwa kikiuka baadhi ya taratibu zilizowekwa na halmashauri
Akizungumza katika Baraza la bajeti la madiwani manispaa ya Iringa meya wa manispaa ya Iringa amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa msaada mkubwa unaotolewa na bajaji bado Kuna sababu ya kufuata Sheria zilizowekwa
Alisema kuwa hapo mwanzo kulikuwa na maombi yaliyotolewa na madereva bajaji wakayapokea hivyo madereva bajaji wanakila sababu ya kusimamia ombi la kutengewa barabara zao na kupitia katika maeneo waliyoyaomba
Alisema kuwa pamoja na kufanyika kwa vikao zaidi ya kumi kati ya halmashauri na madereva bajaji na daladala bado havijaa matunda kutoka uwepo wa baadhi Yao wanaovunja Sheria " nataka niseme kwamba tumekuwa tukizungumza Sana na Hawa vijana wa bajaji lakini wengi wao wamekuwa wakivunja Sheria na kwenye kinyume na makubaliano"
Katika hatua nyingine meya wa manispaa ya Iringa aliitaka ofisi ya mkurugenzi na afisa biashara kuwachukulia hatua madereva bajaji wanaovunja Sheria zilizowekwa
Hata hivyo alimtaka mkurugenzi kutopokea taarifa za bajaji kutoka kwa diwani yeyote anayetetea bajaji badala yake taarifa zote zitolewe kwenye ofisi ya meya . "Naomba nikuagize mkurugenzi pamoja na ofisi ya biashara kuwachukulia Sheria madereva bajaji wote wanaovunja Sheria kwa sababu hii ni changamoto pia daladala hizi zimekuwa zikitusaidia kusafirisha watoto wetu kutokana na uwepo wa vitendo vya ubakaji ambavyo vimekuwa vikifanyika katika jamii zetu "alisema
MWISHO .
Post A Comment: