Na,Elizabeth Paulo Dodoma


Katika kutekeleza Mpango mkakati wa Majukumu mbalimbali ya Bodi ya Maji Bonde la Mto Ruvu imepanga kujenga zaidi ya Visima 10 katika mikoa ya Morogoro na  Pwani  ili kubakabiliana na changamoto za maji zinazokumba maeneo hayo.


Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibarik Mmasi jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu yanayofanywa na Bodi hiyo na kusema wamekuwa wakitoa vibali kulingana na mahitaji huku wakisimamia vyanzo vya maji kwa maendleo endelevu.


Aidha amesema bodi hiyo imekuwa ikidhiti utoaji maji taka katika viwanda ili kuyaboresha maji hayo yatumike kwa matumizi mengne na kuepukana na uchafunzi wa mazingira sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji .


“Lengo la kuanzishwa kwa bodi ya maji ni pamoja na kuhakikisha rasilimali za maji zinalindwa,kutunzwa na kuendelezwa  kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho sambamba na kuhakikisha utunzaji wa mazingira,”amesema.


Pia amebainisha mafanikio yaliyofanywa na bodi hiyo ikiwemo kukarabati na kuboresha miradi sugu ya visima vilivyoanzishwa kwa muda mrefu.


Pia Mmasi amesema kuwa Bodi ya maji imeweza kufanikiwa  kubaini  vyanzo vipya vya maji ambavyo amevitaja kuwa ni eneo la Nzuguni lililopo Jijini Dodoma kuwa linamaji ya kutosha na hivi karibuni litatangazwa katika gazeti la serikali kuwa ni benki ya maji pamoja na Dakawa katika mji wa Dodoma.


Kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji mhandisi Mmasi amesema kuwa wanahakikisha vyanzo vyote vinatunzwa kwa ajili ya kutunza maji yaliyopo chini ya Ardhi huku akiwataka watanzania kuepukana na tabia ya uchimbaji ovyo wa visima vya maji kwa maelezo kuwa kunaweza kusababisha kuchafua maji yaliyopo chini ya ardhi jambo ambalo ni hatari kuweza kuondoa sumu ambayo inaweza kujitokeza.


Hata hivyo ameitimisha kwa kutoa rai kwa watu  wanaochimba visima holela na kuwataka wanachi kutoa taarifa ya visima hivyo ili kuepuka madhara yanayojitokeza kutokana na maji yasiyopelekwa maabara kufanyiwa vipimo.

Share To:

Post A Comment: