Na Denis Chamb, Tanga.
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Tanga kimeamua kwa kauli moja kulitaka jeshi la polisi jijini Tanga kumkamata na kumfikisha katika vyombo vya sheria mlinzi wa shule ya sekondari Marungu ambaye anadaiwa kusababisha moto uliounguza jengo la ofisi ya utawala ambapo nyaraka na vyeti mbalimbali vimeteketea kwa moto.
Akitoa taarifa hiyo kikaoni hapo Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo amesema kwamba mlinzi huyo anadaiwa kuchoma moto jengo hilo akiwa katika harakati za kufukuza nyuki ambao walitanda katika eneo hilo la shule kulingana na maelezo ya mlinzi huyo moto huo ulizuka gafla katika shule hiyo na kuenea hadi katika jengo hilo la utawala ambapo ulichoma nyaraka muhimu na vyeti vilivyokuwa vimehifadhiwa katika jengo hilo.
Taarifa zilizopatikana baadae zimeeleza kuwa baadhi ya nyaraka hizo ni pamoja na risiti za manunuzi na vifaa kwajili ya ujenzi shuleni hapo.
Uongozi wa Halmashauri ya jiji la Tanga una wasiwasi na kuzuka kwa moto wa gafla shuleni hapo wakiamini jambo hilo ni moja ya hujuma zilizofanywa kwa ushirikiano kati ya watumishi wa shule hiyo na mlinzi huyo.
Awali Mstahiki Meya huyo alizungumzia kuhusu taarifa za, hujuma zinazofanywa, na, baadhi ya watumishi waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia miradi ya ujenzi hasa ya madarasa ambapo ameeleza kwamba kuna mahali pamejengwa darasa linalodaiwa kugharimu milioni 20 lakini halina samani ndani yake na hivyo ameonya jambo hilo na kusema uongozi wa Halmashauri hautafumbia macho jambo hilo.
Katika kikao hicho baraza hilo limeazimia kujenga shule ya sekondari katika kata ya Makorora yenye majengo ya gorofa kulingana na ufinyu wa eneo husika kabla ya 2025 kata hiyo iwe na shule ya sekondari na hivyo kuhitimisha lengo la Halmashauri ya jiji la Tanga kuwa kila kata angalau iwe na shule moja ya sekondari.
Hata hivyo kwenye kikao hicho Mstahiki Meya alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji hilo Dkt. Spora Liana kwenda kuvunja nyumba ya mwananchi mmoja ambaye amejenga ndani ya eneo la barabara inayotoka Ikulu ndogo ya Tanga kwa sababu mwenye kiwanja hicho tayari ameshakabidhiwa kiwanja kingine ili aweze kujenga nyumba katika eneo jingine.
Aidha baraza hulo limetoa muda wa miezi mitatu kwa wamiliki wa majengo yote ambayo yamekuwa ni mabovu kwa kipindi cha muda mrefu aidha kuyauza au kuyafanyia marekebisho ili kuendana na kulinda hadhi ya jiji hilo.
"Majengo mabovu machafu , yaliyochoka katikati ya jiji yanayoharibu taswira ya ya jiji yanatakiwa miezi mitatu aidha yafanyiwe uwekezaji yauzwe au yarekebishwe ili yaendane na hadhi ya ya jiji letu" alisema Shillow.
Katika hauta nyingine baraza hilo limewataka na kuwaelekeza kuwaelekeza wamiliki na wasafirishaji wote wa abiria wanaotoka ndani ya jiji hilo kumalizia safari zao pamoja na kupitia katika stendi kuu ya mabasi.
"Wasafirishaji wote ndani ya jiji la Tanga mnaelekezwa kwamba ni lazima muanze na kumalizia safari zenu kwa kupitia katika stendi ya jiji Kange na kwa wale wenye vituo ambao wamekidhi vigezo ni lazima wapitie wajipange dakika 15 kabla ya muda wa kuondoka na ni lazima wote wapite kange hilo lifanyiwe kazi na yote yanayoyotokea barabara ya Korogwe" alisema Shillow
Pamoja na hayo aliyeteuliwa kuwa diwani wa kata ya Mnyanjani katika uchaguzi mdogo ulifanyika hivi karibunj Simba Kayaga ameapishwa kayika baraza hilo ili kuanza kuwatumikia wananchi.
Post A Comment: