Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Leonard Mchau,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi 14 wanaotarajiwa kustaafu yaliyofanyika Januari 27,2023 Mjini Morogoro.
Sehemu ya Washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Leonard Mchau,wakati akifunga mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi 14 wanaotarajiwa kustaafu yaliyofanyika Januari 27,2023 Mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Leonard Mchau,akimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukuzaji Tija Bw. Yohana Madadi,wakati wa mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi 14 wanaotarajiwa kustaafu yaliyofanyika Januari 27,2023 Mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukuzaji Tija Bw. Yohana Madadi (kulia) akimpongeza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Leonard Mchau mara baada ya kufunga mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi 14 wanaotarajiwa kustaafu yaliyofanyika Januari 27,2023 Mjini Morogoro.
Mshiriki wa Mafunzo kutoka EWURA CCC,Mhandisi Goodluck Mmari,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Leonard Mchau,mara baada ya kufunga mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi 14 wanaotarajiwa kustaafu yaliyofanyika Januari 27,2023 Mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Leonard Mchau,akimkabidhi cheti Mshiriki Mariam Mbaga kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kufunga mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi 14 wanaotarajiwa kustaafu yaliyofanyika Januari 27,2023 Mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Leonard Mchau,aakiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufunga mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi 14 wanaotarajiwa kustaafu yaliyofanyika Januari 27,2023 Mjini Morogoro.
.................................
Na Mwandishi Wetu, Morogoro.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, kupitia Kitengo cha Ukuzaji Tija kimetoa mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi 14 wanaotarajiwa kustaafu, huku wakiaswa kuwa waangalifu kwenye miradi watakayowekeza ili isiwe chanzo cha msongo wa mawazo.
Akifunga mafunzo hayo ya siku tano, kwa watumishi hao kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bodi ya Wakandarasi Tanzania, Bodi ya Watalii na EWURA CCC,leo Januari 27, 2023, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi hiyo, Leonard Mchau, amesema watumishi wanapostaafu huhamasishwa kutumia mafao yao kuwekeza kwenye miradi ambayo haina tija na hawana uzoefu nayo na matokeo yake mafao kupukutika.
“Huko mnakokwenda kuna sheria na taratibu zake niwaombe aina ya uwekezaji mnaokwenda kuwekeza, mjue sheria na taratibu. Ni muhimu nidhamu ya matumizi ya fedha, muwe na mahusiano mazuri, msiwe wahalifu,”
Naye, Mkurugenzi wa Kitengo hicho, Yohana Madadi, amesema kitengo hicho ndio chenye wajibu wa kutoa na kuratibu mafunzo hayo kwa taasisi na idara za serikali na za Sekta binafsi.
“Mafunzo haya tunayatoa ili kumuandaa mfanyakazi na maisha ya kustaafu, na akistaafu bado tunamlea hadi atakapofariki dunia, ndio maana ni wizara ambayo ina dhamana ya kutunza na kusimamia mifuko yote ya hifadhi ya jamii, ikiwamo wa PSSSF upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, kwa hiyo tunatekeleza lengo la wizara yetu yenye dhamana ya mifuko"
Amebainisha kuwa washiriki wamejifunza masuala ya ujasiriamali, mafunzo ya pensheni, usimamizi wa fedha, afya, kilimo, ufugaji na kupanga biashara.
Akitoa neno la shukrani, Mshiriki wa mafunzo hayo, Mhandisi Goodluck Mmari, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao na kushauri kitengo hicho kuweka utaratibu wa kuyatoa Mafunzo hayo mapema baada ya watumishi kuajiriwa ili kujiandaa na kustaafu na kujiwekea akiba.
Kitengo cha Ukuzaji Tija (PPU) chini ya ofisi hiyo ni matokeo ya mabadiliko ya lililokuwa Shirika la Tija la Taifa (NIP), kinatekeleza majukumu yanayolenga kukuza tija na ubunifu kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi.
Post A Comment: