Mbunge akipata maelezo ya maendeleo ya mradi wa maji kutoka kwa Mhandisi Rashidi Shabani.
Na Hamida Kamchalla, MUHEZA.
SERIKALI kupitia mradi wa maji wa miji 28, imetenga sh bilioni 40 katika Wilaya ya Muheza ambazo zitatatua kero ya upatikanaji wa maji wilayani humo na kufikia asilimia 100 ya upatikanaji wa huduma hiyo.
Mbunge wa Muheza Hamisi Mwinjuma ameyasema hayo wakati akitembelea miradi ya maji inayotekeleza na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (Tanga UWASA), na kwamba miradi inayoendelea kujengwa itapunguza kwa kiasi kikubwa hali ya upatikanaji wa maji wilayani humo.
Aidha amesema kwa mradi wa miji 28 mkandarasi tayari ameshabaini mahali ambapo yatawekwa matanki kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo na wanatarajiwa kwamba utekelezaji utaanza mapema mwezi huu wa kwanza na pia utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa.
"Kitu kimoja tunacho ngoja ni ujenzi wa mradi wa miji 28 ambao na sisi Muheza tupo maana Mkandarasi ameshakufa amekagua na kujua matanki yatawekwa wapi, na kwa Muheza garama za mradi ni sh bilioni 40, kwahili nimshukuru Rais wetu Samia Sulluhu Hassan kwa kuwezesha kusainiwa mradi huu" amesema.
"Ili kuhakikisha angalau maji kiwango chake kinaongezeka na vile tumesafisha mahali hapa ili kujenga mtambo wa kusafishia maji kwahiyo tuna imani yataongezeka, lakini pia tuna miradi mingine ya maji ambayo inaendelea"
"Mji wetu unaongezeka pia tulikuwa na tatizo la majitaka lakini kule kilapura tuna mradi wa majitaka na tuna mfumo uleule kusanyaji majitaka, tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Maji ilituletea sh bilioni 1kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kukusanya majitaka na mpaka sasa ujenzi upo kwenye asilimia 40 ya ukamilikaji wake" amebainisha.
Mbunge huyo amebainisha kwamba mbali ni miradi hiyo, upo mradi wa maji ambao unatokea NHC na kusambaza maji kupitia Mdote, Ngwaru hadi Shaurimoyo lakini pia unasambaza maji Muheza nje na ndani.
"Tulikuwa na tatizo la umeme kwa kipindi kirefu kidogo, pamoja na kwamba mradi umefanyika kwa kiasi kikubwa lakini umeme ulikuwa mdogo hauna uwezo wa kusukuma maji, lakini sasa mvua zimeanza kuonyesha tatizo la umeme linaelekea ukingoni na kwa kiwango cha mradi ulipofika kwa miradi tuliyojenga unakwenda kuimarika" amebainisha.
"Kwahiyo mimi niwashukuru watendaji wetu hasa Tanga UWASA wanafanya kazi nzuri na wako na sisi katika mapambani dhidi ya tatizo hili na kuhakikisha tatizo la maji katika Wilaya yetu linakwenda kwisha" amesema.
Naye mkurugenzi wa usambazaji maji na Usafi wa mazingira Tanga UWASA, Mhandisi Rashidi Shabani amesema miradi inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya ya Muheza itasaidia kufikia asilimia 90 ya upatikanaji wa maji hadi kufikia mwezi julai mwaka huu.
"Tumeshapata mkandarasi na sasa yuko kwenye hatua ya maandalisi muda sio mrefu uchambaji wa mtari utaanza ili tuborwshe upatikanaji wa maji kutoka usambazaji wa mwendo wa mitabza ujazo 1500 kwa saa ya sasa hivi hadi kufikia 2000",
"Na kwa mradi huu hata wale watu wa utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta wakichukua mita za ujazo 200 kwa siku itabaki 1800 ambayo itawatosheleza kabisa watu wa Muheza kwa maana watakuwa na maji ya kutosha, hizi awamu ya kwanza na ya pili tumepanga kuboresha upatikanaji wa maji,
"Awamu ya kwanza tuliotoa asilimia 34 lakini imetufikisha asilimia 65, tumeanza awamu ya pili sasa tumelenga mpaka ikifika julai mwaka huu tutoke hapa kwenye asilimia 65 tufike hadi asilimia 85, lakini pia tuna awamu ya tatu ya mradi ambayo hii tumelenga tufikie asilimia 100, na kama siyo basi angalau hata tufikie asilimia 95" amebainisha.
Mbunge akitoa maelekezo kwa Mhandisi katika eneo la kuweka mtambo wa kusafisha maji Magoroto.
Post A Comment: