Diwani wa kata ya Mapanda Obadia Kalenga akishuhudia kazi ya ujenzi wa barabara ya Ukami hadi Mapanda kilometa 31 ikiendelea kujengwa kwa kiwango cha changarawe na kutatua changamoto za wananch
Diwani wa kata ya Mapanda Obadia Kalenga akiwa katika picha na baadhi ya wananchi wa kata ya Mapanda wakishuhudia ujenzi wa barabara hiyo ya Ukami hadi Mapanda kilometa 31
Na hii ndio barabara ya Ukami hadi Mapanda kilometa 31 inayojengwa kwa lengo la kuchochea shughuli za kimaendeleo kwa wananchi wa kata ya Mapanda.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
WANANCHI wa kata ya Mapanda Tarafa ya kibengu wilaya ya Mufindi wamempongeza diwani wa kata hiyo kwa kupambana kuhakikisha anatatua tatizo la barabara ya Ukami hadi Mapanda yenye urefu wa kilometa 31.
Wakizungumza wakati mkandarasi akiendelea ujenzi wa barabara hiyo wananchi hao walisema kuwa barabara hiyo ilikuwa inakwamisha maendeleo ya wananchi wa kata ya Mapanda.
Wananchi hao walisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo Kutachochea shughuli za kiuchumi kwa kurahisisha usafi wa wananchi na wafanyabiashara mbalimbali.
Walisema kuwa Wananchi wa kata ya Mapanda wanategemea kilimo cha mazao ya miti katika kukuza uchumi wao hivyo barabara hiyo ikiwa mbovu hawawezi kusafirisha mazao hayo kwenda sokoni.
Walisema kuwa wanampongeza diwani huyo kwa kupambana kuhakikisha inapatikana bajeti ya ujenzi wa barabara hiyo ya Ukami hadi Mapanda.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mapanda,Obadia Kalenga alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo Kutachochea kasi ya maendeleo ya wananchi kwa kurahisisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wote.
Alisema kuwa anaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo inategemewa na wananchi katika shughuli za kimaendeleo na kiuchumi.
Post A Comment: