Wanafunzi takriban 170 wasio kuwa na uwezo waliotakiwa kujiunga na Elimu ya Sekondari Wilayani Monduli wamepatiwa msaada wa Baadhi ya vifaaa vya Shule vikiwemo Magodoro, Masanduku(tranga) kutoka Ofisi ya Mbunge.


Akizungumza katika Makabidhiano ya vitu hivyo Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Frederick Lowassa amesema zoezi Hilo ni utamaduni wa Ofisi yake na hiyo imeenza baada TU ya kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo Hilo Kwa kuwasaidia watoto waliomaliza shule za misingi mahitaji Kwa baadhi yake kuelekea Sekondari.

''kwa kutambua umuhimu wa Elimu Kwa Jimbo la Monduli kuwa ni kitovu Cha nchi , nimeona iwe desturi ya ofisi yangu kuwasaidia baadhi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la Saba ambao hawatakuwa na uwezo wakati wa kujiunga na elimu Yao ya sekondari kuwasaidia angalau SQbaadhi ya Mahitaji Yao kama mlivyoona magodo , sanduku'' Amesema mbunge


" Sisi wafugaji tumezaliwa na tunaishi Kwa kuamini katika mifugo Mingi kuwa ndio utajiri wetu (bank) Mvua ikinyesha maji yakatitirika tunatamani mifugo ndio wanywe kwanza na sisi ndio tufuate, lakini niwaambie  Pamoja na yote Ardhi haiongezi ila sisi tunaongeza tuwapeleke watoto shule ili baadaye iwe urithi wao tuwasomesheni watoto" Amesema mbunge


Aidha katika Makabidhiano hayo Frederick ameongeza Kwa kuwaomba viongozi wa Mila Kwa kushirikiana na Walimu wakuu kuhakikisha Kila mwanafunzi aliyepangiwa kujiunga na Elimu ya sekondari kuripoti shuleni mapema na asiwepo wa kubaki Kwa namna Moja au nyingine.


Wakati huohuo baadhi ya wanafunzi waliopatiwa msaada huo pamoja na wazazi wao wameishukuru ofisi ya Mbunge Kwa Msaada huo na kusema Kwa sasa wataripoti Shuleni kwani Awali kwa baadhi Yao bado hawajaripoti.


Thomas Lukumai ni Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Olesokoine , amesema pamoja na Hamasa kuwepo kwa wazazi juu Elimu Bado ukame ni changamoto katika utekelezaji wa mahitaji ya watoto Kwa jamii hiyo .

" Hamasa ni kubwa sana Kwa wazazi kuwapeleka watoto shule tatizo ni Ukame unawakwamisha , mifugo wanakufa Kwa hiyo Hadi January ifike mzazi anakosa kitu Cha kuuza Kwa ajili ya mtoto wake , kwa shule yangu ya Olesokoine waliotakiwa kuripoti bado nusu hawajaripoti na hili linawezekana ni watoto kukosa mahitaji , lakini kama mwanafunzi atakuwa na sare ya Shule hata pea Moja na madaftari yake tutampokea wakati Mzazi akiendelea kujipanga"". Amesema Mwalimu Lukumai

Share To:

Post A Comment: