Waagizaji,wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa za chuma nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa bidhaa wanazoingiza ni zile zinazokidhi vigezo vyote vya ubora kwa mujibu wa viwango vya kitaifa na kuzingatia taratibu zote za uingizaji hapa nchini.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, wakati wa ufunguzi wa kikao kati ya TBS hiyo na waagizaji na wasambazaji wa bidhaa za chuma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania TBS, Dkt Candida Shirima, amesema kuwa kila mzalishaji wa bidhaa hizo anatakiwa kuhakikisha anazalisha bidhaa zinazokidhi vigezo vyote vya ubora kwa mujibu wa viwango.
Aidha Dkt Shirima amesema kuwa bidhaa hizo zinatakiwa kuandikwa taarifa zote muhimu ambapo kwa mujibu wa viwango cha kitaifa zinazotakiwa kuandikwa kwenye bidhaa hizo ni grade ya bidhaa, jina la mzalishaji,vipimo na namba ya toleo
Katika hatua nyingine TBS imesema itaendelea kutekeleza kikamilifu jukumu la kuhakikisha ubora wa bidhaa hizo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuzifanyia ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara kabla ya kuingia nchini na wakati zinapokuwa katika soko,kufanya ukaguzi wa viwanda vya uzalisahaji na kudhibitisha ubora wa bidhaa zinazozalishwa ,kufanya ufuatiliaji katika soko mara kwa mara ,kutoa elimu na kuchukua hatua stabilizer kwa wale wote wanaokiuka matakwa ya Sheria.
Post A Comment: