SERIKALI imefungua mjadala wa utekelezaji wa mradi wa uhimarishaji salama ya Miliki za Ardhi yaani ‘Land Tenure Improvement Program’.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akizungumza na HabariLeo, leo Januari 18, 2022 amesema kuwa mradi huo unakwenda kupima, na kutambua vipande vya ardhi katika Mikoa 16 na Halmashauri 41.
Amesema pia ujenzi wa miundombinu ikiwemo majengo ya makamishna wa ardhi mikoa yote ya Tanzania Bara na kufunga mifumo ya kiteknolojia kwa ajili ya kurahisisha upimaji na utambuzi katika utawala wa Ardhi.
Ridhiwan amesema, gharama ya mradi mzima ni Shilingi Bilioni 345 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Dunia
Post A Comment: