Vijana wametakiwa kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya ukatili wa kijinsia hususani Kwa watoto wa kiume ambao hawapasi sauti.
Hayo yamebainika wakati wa Maadhimisho ya Miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi CCM iliyofanywa na Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha 30 January 2023 ,Kwa kufanya ziara pamoja na matembezi, kupanda miti katika chuo Cha Maendeleo Monduli, Hospital ya wilaya ya Monduli, pamoja na kugawa mahitaji mbalimbali Kwa wagonjwa hususa hodi za watoto, wajawazito, pamoja na wazazi.
Akiongoza Maadhimisho hayo Mwenyekiti wa UWT Bi Agnes Mrefu amewaasa vijana hususani wa kiume kujilinda dhidi ya ukatili.
" Pamoja na Maadhimisho hayo CCM imefanya mambo mengi na mazuri ya kimaendeleo lakini niwaombe wanawake pamoja na watoto wa kiume jilindeni ,lindeni miili yenu watoto wa kiume wanafanyiwa ukatili mno lakini Kwa kuwa hakuna pa kusema au pengine wanaogopa kusema itatusababishia kuwakosa wababa lakini pia walezi wa familia kizazi kijacho" amesema Agnes Mrefu .
" Leo tumepanda miti hapa tunaomba viongozi wa chuo hiki kulinda Ili mwaka ujao turudi tukute miti zote zipo hai" Agnes Mrefu.
Epiphania Massage ni Muuguzi Mfawidhi (Matron) Amewaongoza wanawake hao katika kugawa mahitaji mbalimbali Kwa wagonjwa mbali TU na kuwashukuru ametoa Elimu juu chanjo ya UVICO 19 akiwasihi wanawake hao kuchanja kwani Bora kinga kuliko tiba ,pamoja na chanjo ya Ini akiwasihi kujilinda, kuwalinda wengine bila kusahau chanjo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Katibu wa CCM Monduli Bi Rukia , Ambapo Wamefanikiwa kuwaingiza wanachama wampya 150, huku jumla ya miti iliyopandwa ni jumla ya 150.
MIAKA 46 YA CCM "KAZI IENDELEEE"
Post A Comment: