Na Mashaka Kibaya, Tanga.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary
Chatanda amepongeza hatua ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kuondosha
zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya Siasa akisema,imerejesha faraja kwa
wananchi na wapenda amani.
Akiwa katika mkutano wake na wanahabari jana Jijini Tanga, Chatanda
alisema, UWT inampongeza Dkt Samia kwa kufanya maamuzi yaliyoleta furaha isiyo
na kifani kwa wananchi na wapenda amani.
Chatanda alisema kwamba, hatua hiyo imetoa majawabu kwa demokrasia ya nchi akitaja
uondolewaji mikutano ya hadhara, kukwamua mchakato katiba mpya,kufanya
marekebisho sheria mbalimbali ili kupanua wigo wa demokrasia.
"Maamuzi ya Rais Dkt Samia yameleta faraja kwa vyama vya siasa na
hatawapenda amani wote, ameonesha uthabiti wa kauli zake kwa
matendo"alisema Chatanda.
Aidha Chatanda amesisitiza umuhimu wa vyama vya siasa kufanya mikutano yake
bila lugha za matusi kwa maelezo kuwa ni muelekeo mpya wa nchi katika kuihami
demokrasia.
"Mama Samia ni neema kutoka kwa Mungu matumaini mapya yamerejea katika
kujenga demokrasia,UWT inaungana naye, kilio cha UWT ni kuona amani
inatawala" alisema Chatanda.
Mwenyekiti huyo wa UWT amesisitiza umuhimu wa amani na utulivu kuendelea
kutawala ili kutoa fursa kwa Rais Dkt Samia kuendelea kushughulika na kero za
wananchi.
Amewataka viongozi wa UWT kufanya mikutano ya hadhara kwa kufuata taratibu
zote akiwahimiza kusikiliza kero zote kwa lugha ya kistaarabu.
Katika mkutano huo pia Mary Pius Chatanda alitumia wasaa huo akiahidi kutoa
shilingi Milioni moja kwa ajili ya kikundi cha hamasa kinachotoa mchango mkubwa
kuhamasisha maendeleo.
Alisema amewiwa kutoa mchango wake huo baada ya wahamasishaji hao kuwa na
mchango mkubwa kwa shughuli za chama na Serikali.
"Hata kipindi cha Mwalimu alikuwepo bibi Titi aliyekuwa akitangulia
kwakuimba na kuzungumza kidogo halafu ndipo akawa anamkaribisha
Nyerere"alisema Chatanda.
Chatanda amebainisha kuwa fedha hizo kwa kikundi hicho cha
hamasazitawasaidia kujianzishia shughuli za kiuchumi na kuweza kujikwamua.
Post A Comment: