Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Ilemela Ndugu Salum Mtaturu akizungumza na vijana waliohitimu mafunzo ya itifaki na hamasa wilaya ya Ilemela hawapo pichani
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mwanza Ndugu Seth Bernard Masalu akiwa pamoja na viongozi wengine kwaajili ya kuimba wimbo wa taifa
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mwanza Seth Bernard Masalu akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya itifaki na hamasa kijana wa wilaya ya Ilemela
Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mwanza Comred Seth Bernard Masalu ameupongeza uongozi wa Jumuiya ya vijana wilaya ya Ilemela Kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuimarisha Jumuiya hiyo ngazi ya wilaya na usimamizi mzuri wa Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.
Akizungumza katika hafla ya kufunga Kambi la mafunzo ya itifaki na uhamasihaji ngazi ya wilaya iliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Kiloleli Comred Seth amesema kuwa kazi inayofanywa na viongozi wa wilaya hiyo ni ya kuigwa na kuungwa mkono huku akiwataka viongozi wa wilaya za jirani kuiga mfano wao
‘.. Kazi mnayoifanya ni kubwa na niwatie moyo uongozi wa mkoa unawaunga mkono na upo pamoja na nyie katika jambo lolote la maendeleo mtakalolifanya ..’ alisema
Aidha Comred Seth amewataka vijana wa wilaya ya Ilemela kuendelea kujitoa kwaajili ya chama chao pamoja na kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kunufaika na fursa za kiuchumi zinazohitaji vijana.
Kw upande wake Katibu wa Jumuiya ya vijana wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Joshua Kandumila mbali na kuwapongeza vijana waliofuzu mafunzo ya itifaki wilaya ya Ilemela amezitaka wilaya nyengine zilizopo ndani ya mkoa huo kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yaliyotolewa na mkoa juu ya kuhakikisha Kila wilaya linafanya kazi ya mafunzo Kwa vijana wake.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa CCM wilaya ya Ilemela Comred Salum Mtaturu amewataka vijana wa wilaya hiyo kujiunga katika vikundi Ili waweze kunufaika na fursa ya mikopo ya asilimia nne Kwa vijana inayotolewa na halmashauri Ili waweze kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayowakwamua kimaisha.
Zaidi ya vijana 478 wamefuzu mafunzo ya itifaki na hamasa wilaya ya Ilemela kutoka katika kata 19 za wilaya hiyo
Post A Comment: