Na Denis Chambi, Tanga.
MAHITAJI wa walimu kwa mkoa wa Tanga katika sekta ya elimu kwa upande wa shule za msingi na sekondari bado ni makubwa ili kukidhi ongezeko la wanafunzi waliopo kwa muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2023 ambapo kwa upande wa shule za msingi kuna upungufu wa walimu elfu tano mia moja kumi na tisa (5,119) wakati huo huo sekondari zikihitaji walimu elfu moja mia moja ( 1,100) .
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika sekta ya elimu kwa mkoa huo ambapo amesema kuwa kuna ongezeko kubwa la wanafunzi kwa mwaka huu na uhitaji mkubwa zaidi kwa upande wa shule za sekondari ni katika masomo ya sayansi na hisabati.
" Kama mnavyofahamu ubora wa elimu sio majengo peke yake, ubora wa elimu ni pamoja na idadi ya walimu kuongezeka mkoa una jumla ya wanafunzi wa shule za msingi laki tano kumi na nne mia saba kumi na nane ( 514, 718) wakiwemo wavulana laki mbili hamsini tisa mia saba ishirini na saba (259 ,727) na wasichana ni laki mbili hamsini na nne mia tisa hamsini na moja (254, 951) kuanzia elimu ya awali hadi darasa la saba" alisema Mgumba
"Pia kwa upande wa shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita zina jumla ya wanafunzi laki moja kumi na moja mia moja thelasini tano (111,135 ) wakiwemo wavulana elfu arobaini na tisa mia tisa sitini na saba (49, 967) na wasichana elfu sitini na moja mia moja sitini na nane (61, 168)"
"Mahitaji ya walimu wa shule za msingi yaliyopo ni walimu elfu kumi na tatu mia tisa na sitini (13,960) waliopo sasa ni elfu nane mia nane arobaini na moja (8, 841) na upungufu ni elfu tano mia moja kumi na tisa (5,119) na kwa shule za sekondari zina uhitaji wa walimu elfu sitini na moja mia moja sitini na tisa (6169) waliopo ni elfu tano na sitini na tisa 50,69 huku upungufu ukiwa upungufu ni ( 1,100) na upaungufu kwa sekondari ni katika masomo ya sayansi na hisabati na hatuna upungufu katika masomo ya sanaa " alieleza Mgumba.
Aidha alieleza kuwa licha ya uhaba huo ili kuendelea kupunguza changamoto iliyopo kwa mwaka 2022/2023 serikali tayari imeshaajiri walimu wapya wapatao mia saba sabini ambapo kwa shule za msingin ni walimu mia nne arobaini na tatu ( 443) huku sekondari wakiwa ni mia tatu ishirini na saba (327) .
"Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia walimu wapya 443 wa shule za msingi na 327 wa shule za sekondari mwak 2022/2023 ambao wamepunguza changamoto ya uhaba wa walimu katika shule zetu na uhaba huu mkubwa umekuja kutokana na kasi kubwa ya serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu " alisema
Hta hivyo mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa malengo yaliyopo kwa sasa ni kutaka kuondoa kabisa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya kitaifa kwa daraja la nne wakibakisha daraja la kwanza mpaka la tatu huku akiwaelekeza waratibu maafisa elimu na viongozi wote kuhakikisha wanafanya tathmini ya kutaka kujua ni kwa kias gani wanaweza kutimiza malengo hayo
"Malengo yetu kama serikali ya mkoa wa Tanga ni kuhakikisha ufaulu ndio tumefika katika asilimia 81 lakini sasa nimewaelekeza waratibu wa elimu , maafisa elimu na voingozi wote wachambue ufaulu huo ni wa daraja gani kwa kiasi gani malengo yetu watoto wanaofaulu kuanzia daraja la kwanza mpaka la tatu wasipungue asilimia hamsini 50 katika mkoa wa Tanga kwa sababu tukiwa na ufaulu huo mwanafunzi anaweza kuendelea na elimu ngazi za juu ikiwemo vyuo ".
Pamoja na hayo mkuu huyo wa mkoa amesema serikali imekuja na mpango wa "BOOST" unaolenga kuboresha miundombinu ya elimu kwa shule zote za msingi akiwataka wataalamu wa elimu kuainisha shule zote kongwe zenye miundombinu chakavu ili ziweze kukarabatiwa.
"Serikali kuanzia mwezi wa kwanza mwishoni tutaanza na mradi mkubwa unaitwa Boost wa uboreshaji miundombinu ya elimu shule za msingi tumeshawaelekeza wataalamu wetu wa elimu kuainisha maeneo ambayo shule za tangu Mkoroni hazijawahi kufanyiwa maboresho wala matengenezo na kama kunahitajika maboresho yafanyike maboresho makubwa na zipi zinahitaji kubomolewa ili tuanze ujenzi upya "
Post A Comment: