Taasisi isiyo ya kiserikali ya Usambara Development Initiative(UDI) iliyopo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imejipanga kusaidia na kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu ikiiunga mkono serikali katika kuwatafutia maendeleo wananchi.
Taasisi hiyo ya UDI ambayo inaundwa na wananchi wazawa wanaoishi ndani na nje ya wilaya ya Lushoto ikiwa na dhamira thabiti ya kuinua kiwango cha elimu na kuongeza ushindani kwa wanafunzi kutoka shule za serikali za msingi na sekondari imedhamiria kutoa tuzo mbalimbali kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwnye mitihani yao ya kitaifa .
Mkuu wa wilaya ya Lushoto Karist Razaro ameihakikishia ushrikiano taasisi ya Usambara katika kuhakikisha inaunga mkono jitihada za serikali kupitia nyanja mbalimbali huku akiwataka kufwata taratibu sheria na kanuni walizojiwekea ili kuweza kutimiza malengo yao.
"Nimeendelea kusisitiza kwamba taasisi za kijamii kama hizi sio washindani wa maendeleo ya serikali bali wao ni washirika wa serikali hivyo serikali yetu ya Lushoyo itaendelea kushirikiana na wao na taasisi zingine ili kuleta maendeleo kwa wilaya yetu, niwaombe tu waendelee kufwata kanuni na katiba yao ipasavyo ili yale malengo ambayo wameyakusudia ya kusaidiana na serikali kuleta maendeleo yaweze kutimia" aliongeza Razaro
Awali akizungumza mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya UDI Muna Gogola amesema kuwa malengo yao makubwa ni kutaka kuona wanashiriki kikamilifu kusaidia jamii zilizopo ndani ya wilaya ya Lushoto hasa kupitia sekta za elimu afya pamoja na kufungua na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana akiwataka wanachama na wadau wote wa maendeleo katika wilaya hiyo kuonyesha ushirikiano wa hali na mali ili kuweza kufikia malengo mbalimbali waliyojiwekea .
"Matarajio yetu makubwa ni kuona taasisi inaendelea na kufanya vitu vingi vya kusaidia jamii ya wana Lushoto ikiwemo katika elimu , afya utalii na nyinginezo tukilenga maendeleo kwa ujumla kwahiyo tunatarajia wanachama na wadau wote wa maendeleo ndani ya wilaya ya Lushoto kuwa bega kwa bega na sisi ili kuhakikisha tunaleta maendeleo katika wilaya yetu ya Lushoto" alisema Gogola
Alisema UDI ni muunganiko wa wazaliwa wote wanaotoka ndani ya wilaya ya Lushoto akiendelea kutoa wito kwa wale ambao bado sio wanachama wa taasisi hiyo waliopo nje na ndani kuja kuungana kwa pamoja katika kulisukuma gurudumu la maendeleo kwa hali na mali.
"UDI ni kwaajili ya maendeleo ya Lushoto ambayo yanamgusa mtu yeyote ambaye anaishi katika milima hii popote alipo kwa kuzingatia matakwa na kanuni za umoja wetu anaruhusiwa kujiunga , UDI inalenga kuinua maendeleo katika kila sekta kwahiyo tunagusa maisha ya jamii katika nyanja zote"
Mwenyekiti huyo ameiomba serikali serikali kuiunga mkono taasisi hiyo ili iweze kufikia malengo yake ya kuleta maendelo kwa wananchi wanaoishi ndani ya wilaya ya Lushoto huku wakijipanga kuondoa dhana iliyojengeka ndani ya jamii kuwa wilaya hiyo ni kitomvu cha wasichana wanaofanya kazi za ndani sehemu mbalimbali.
"Ombi letu kwa serikali ni kuwaomba watuunge mkono kwa sababu sisi lengo letu ni kuisaidia serikali kwahiyo pale popote ambapo tutahitaji msaada kutoka serikalini, tunataka pia tuondoe dhana iliyojengeka ndani ya jamii kuwa Lushoto wanapatikana sana wadada wa kazi za ndani , tunataka wazazi wajue kwamba kila mtoto anapaswa kupata elimu na wanapaswa kusimamiwa ili aweze kufanikiwa katika maisha yake, tunahitaji kwenda kuisaidia na kuielimisha jamii" alisema mwenyekiti huyo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchama wa taasisi hiyo Gabriel Bernad na Seveline Baruti wamesema kuwa uwepo wa taasisi hiyo ndani ya wilaya ya Lushoto utasaidia kuibua na kokomesha vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika jamii huku wakiimarisha mifumo ya malezi kwa watoto ambayo inaweza ikaharibu tamaduni na kizazi cha baadaye.
Post A Comment: