RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amefuta sherehe za Mapinduzi na kuelekeza fedha zilizotengwa kwa ajili ya Sherehe hizo za Miaka 59 ya Mapinduzi iliyokuwa zifanyike Januari 12, 2023 zitumike katika sekta ya elimu.
Akizungumza jana Desemba 31, 2022 Rais Dk Mwinyi amesema awali sherehe za Mapinduzi zilipangwa kutumia Sh milioni 700 licha ya gharama kupunguzwa hadi kufikia Sh milioni 450, ambazo amesema serikali imezielekeza kuongeza nguvu kwenye sekta ya elimu ikiwemo madarasa, madawati, maabara na huduma nyingine za elimu.
Post A Comment: