Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Nchini NIMR Profesa Said  Aboud  akizungumza kwenye  kikao cha wadau wa afya kilichofanyika January  25. 2023 mjini Morogoro.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Nchini NIMR Profesa Said  Aboud ( wakwanza kushoto ) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Afya waliokutana  Mjini Morogoro  January 25. 2023.

Na Farida Mangube. Morogoro. 


Serikali imeanzisha mfumo wa kitaifa wa kanzidata ya ukusanyaji wa tafiti za afya utakaosaidia kuweka pamoja tafiti zote zinazofanywa na taasisi za utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini ili kurahisisha upatikanaji wake na kuepusha kurudia kufanya tafiti zilizofanywa na taasisi nyingine.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa sera na mipango Wizara ya afya Edward  Mbanga kwenye kikaokazi cha wadau wa afya ambapo alisema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na mkanganyiko wa upatikanaji wa tarifa sahihi za tafiti za afya ambazo zingewezesha serikali kupanga  mipango endelevu ya sekta ya afya nchini.


"Kwa sasa hakuna kituo maalumu cha kuwezesha upatikanaji wa tafiti za magonjwa ya binadamu kwahiyo mfumo huu ni muhimu hasa katika wakati huu wa ukuaji wa sayansi na teknolojia."  alisema Mbanga


“Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha inaborsha upatikanaji na utoaji wa Huduma za afya nchini lakini pia eneo la afya ni eneo linalokuwa na mabadiliko ya mara kwa mara ili kufanikisha hayo lazima kufanya tafiti kwa mfano kuna magonjwa ambayo yamekuwa yakijitokeza na pengine wataalamu wetu kushindwa kuyafanyia kazi hivyo kuwataka kufanya utafiti ili kuwawezesha kujua hatua gani wanaweza kuchukua dhudi ya magonjwa hayo” aliongeza

Aidha aliwataka watafiti kutafsiri maandiko ya utafiti wanaoufanya kwa lugha ya kingereza kwenda lugha ya kiswaiswahili ili kuwawezesha watanzania ambao hawana uwezo wa kusoma na kuelewa lugha ya kingereza kunufaika na utafiti huo


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Nchini NIMR  Profesa Sid Aboud  amesema mfumo huo unabuniwa na kutengenezwa na wataalamu wa nimr na kwamba taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya afya.


 Naye Mtafit Mkuu Daktari Amos Kahwa  amesema uanzishwaji wa mfumo huu utasaidia sana wizara ya afya pamoja na watunga sera kwani kila atakaye hitaji kutumia tarifa za utafiti aweze kuzipata kwenye kanzidata kwa wakati.


mwisho.




 

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: