Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametoa wiki tatu kwa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Ukerewe kulipa deni la umeme shilingi milioni 65 kwa shirika la umeme nchini TANESCO baada ya kukatiwa umeme hali iliyosababisha wananchi kukosa huduma ya maji.
Mahundi ametoa agizo hilo ikiwa ni siku chache tangu Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango alipofanya ziara wilayani hapo na kushuhudia wananchi wakikosa maji kutokana na kuharibika pampu ya kusukumia maji pamoja na kukatiwa umeme.
Ameipongeza RUWASA kwa namna walivyojituma kurejesha huduma ya maji ili adhima ya Rais ya kumtua mama ndoo kichwani iweze kufikiwa.
Aidha, amewataka RUWASA kuhakikisha wanakusanya ankara za maji ili waweze kujiendesha
Kwa upande wake, Mbunge wa Ukerewe Mhe Joseph Mkundi amefurahishwa na namna uongozi wa Wizara ya Maji wanavyosimamia utekelezaji wa miradi ya maji.
Post A Comment: