Na.OMM Rukwa
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Sumbawanga imefanikiwa kuunganisha vyombo vya watoa huduma za maji ngazi za jamii (CBWSO) toka 46 hadi 11 hatua iliyosaidia kufikisha huduma za maji karibu na wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba amesema hayo leo (Januari 02,2023) mjini Sumbawanga wakati akifungua mkyano wa nusu mwaka wa vyombo vya watoa huduma za maji ngazi ya jamii ambapo ameseamutaratibu huo umesaidia jamii.
“RUWASA Sumbawanga imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa vyombo vya watumia maji baada kuunganisha vyombo 46 hadi kufikia 11 vya sasa hatua iliyowezesha vyombo kuwa na uwezo wa kutoa bili za maji na wataalam” alisema Waryuba.
Waryuba aliongeza kusema uweo wa vyombo vya watumia maji ngazi ya jamii unatarijiwa kuwa na utendaji wenye tija,ubunifu na weledi ili wananchi wengi zaidi wapate maji karibu na ya uhakika kwani serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji.
Katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa na kuwa endelevu Waryuba alitoa agizo kwa watendaji wa kata zote wilaya ya Sumbawanga kuwaondoa wananchi wote wanaolima ndani ya vyanzo vya maji pamoja .
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Sumbawanga Mhandisi Jonas Maganga alisema tangu kuanzishwa kwa vyombo vya watumia maji ngazi ya jamii mafanikio ya makushanyo ya fedha yameongezeka kwenye vijiji 24 vya Manispaa na vijiji 114 vya Sumbawanga vijijini.
Mhandisi Maganga alitaja makusanyo yaliyopatikana kuwa mwaka 2019/20 ( Milioni 12), mwaka 2020/21 (Milioni 129) na mwaka 2021/22 (Milioni 145) hatua inayosaidia vyombo kujiendesha na kupunguza utegemezi wa wa serikali.
Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji maji toka asilimia 51 mwaka 2019/20 hadi kufikia asilimia 71 mwaka 2022/23 kwa wilaya ya Sumbawanga huku serikali ikiwezsha bajeti ya huduma za maji kufikia shilingi Bilioni 5.1 mwaka 2021/22 toka Bilioni 1.3 mwaka 2019/20 kupitia mradi wa Lipa kwa Matokeo (P4R).
Naye Mhasibu wa Jumuiya ya Muze, Salum Msimba alisema uwepo wa vyombo hivyo umesaidia kuongeza uwezo wa kuhudumia wananchi kufuatia uchangiaji huduma za maji ambapo katika mwaka 2021/22 walikusanya shilingi Milioni 23 tofauti na shilingi Milioni 5 mwaka 2019/20.
“Niipongeze Ruwasa kwa kutengeza ajira ,hapa mimi ni mwajiliwa wa bodi ambapo nalipwa kupitia ukusanyaji wa bili za maji “alisema Msimba.
Post A Comment: