Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ameondoa zuio la kufanya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa kwa madai kuwa ni haki yao kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Rais Dk Samia amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 3, 2023 na kuongeza kuwa wajibu wa serikali ni kuwalinda katika mikutano hiyo.

“Wajibu wenu ni kufuata sheria zinavyosema ni kufuata kanuni zinavyosema, lakini kama waungwana kama wastaarabu Watanzania wenye sifa ndani ya dunia hii niwaombe sana, tunatoa ruhusa twendeni tukafanye siasa za kistaarabu, siasa za kupevuka, tukafanye siasa za kujenga sio kubomoa,” amesema Dk Samia

Share To:

Post A Comment: