Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amemuagiza mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kuwakamata wazazi wote ambao hawajapeleka watoto kuanza muhula mpya wa masomo na kuwafanyisha usafi kwenye shule hizo pamoja na vituo vya afya badala ya kuwaweka rumande.


Mtaka ametoa agizo hilo akiwa katika shule ya Sekondari Mbeyela mjini Njombe wakati akikagua zoezi la kuripoti wanafunzi shuleni ambapo katika shule hiyo wameripoti wanafunzi 62 pekee kati ya 300 wa kidato cha kwanza wanaopaswa kuanza masomo.

"Hatuwezi kuruhusu ujinga kwenye suala la elimu nikuagize mkuu wa wilaya ya Njombe kamata wazazi wote ambao hawajawaleta wanafunzi shuleni beba magari ya polisi yote wapakiwe humo ili waje mashuleni kufanya usafii wa vyoo na Madarasa"amesema Anthony Mtaka mkuu wa mkoa wa Njombe

Amesema hakuna sababu ya kuwapeleka rumande wazazi hao wakamalize chakula Cha serikali hivyo wanapaswa kufanya usafi kwani haiwezekani serikali ikajenga madarasa na kufuta ada halafu wazazi washindwe kuwapeleka watoto shuleni.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amekiri kupokea maelekezo ya mkuu wa mkoa na kwenda kuyafanyia kazi.






Share To:

Post A Comment: