Mwenyekiti wa Jimbo la Mikumi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bakari Hasani amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema ameridhika na kazi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na ameamua kumuunga mkono.
“Sijalazimishwa na mtu yeyote sijagombana na ndugu zangu wa Chadema, najua matusi yatakuwa mengi ila hakuna tusi jipya. Nimeona sura aliyoonesha mama Samia kwenye ujenzi wa taifa, acha nije kumuunga mkono, ” amesema Hasani.
Tukio hilo limefanywa leo katika Kijiji cha Dumila Juu wilayani Kilosa, mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akiwa katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Morogoro ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama ngazi ya mashina.
Post A Comment: