Na Denis Chambi ,Tanga.
Mwenyekiti wa chama cha mapinuzi CCM mkoa wa Tanga Abdurahman Rajabu leo january 31 amekabidhi kitita cha shilingi Millioni 20 fedha ambazo ni sehemu ya Million 30 zitakazotumika kununua generator kwaajili ya matumizi ya uwamja wa mkwakwani ambapo sasa mechi zitakazochezwa usiku zitashudiwa mubashara katika uwanja huo.
Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya chama cha mapinduzi ambao pia ni wamiliki wa uwanja huo wa Mkwakwani jumamosi hii kutakuwa na mchezo wa kirafiki utakaowakutanisha mahasimu na watani wa jiji la Tanga Coastal Union 'Wagosi wa kaya' na majirani zao African Sports ' Wanakimanumanu' timu hizo ambazo zina historia ya soka la Tanzania kwani mwaka 1988 Caostal walitwaa ubingwa wa bara huku African Sports wao wakinyakua kombe la Muungano.
Akikabidhi fedha hizo tukio ambalo limeshudiwa na wawakilishi wa Coastal Union pamoja na African Sports mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Abdurahman Rajab amesema kuwa lengo lao kwa sasa ni kufufua utani wa jadi katika michezo kama ulivyokuwa tangu enzi na enzi baina ya timu hizo mbili sambamba na michezo mingine ikiwa pia ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama chao.
Rajabu amesema kuwa anashangazwa kuona kuwa bado kuna wanatanga ambao wanazishabikia timu za nje badala ya zile zilizopo ndani ya mkoa huo kitu ambacho sasa wanataka wakiondoe kwa wapenzi mashabiki na wadau wa michezo na hivyo kuwafanya wawe na mapenzi ya dhati na vya kwao .
"Kwetu sisi kama chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga katika maadhimisho haya tukasema tufanye mambo mengi ya kijamii na jumuia zetu zote tatu zimefanya kama kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum, tukasema miongoni mwa mambo makubwa ambayo tunatakiwa tuyafanye ni kurudisha ari za wanatanga kwa timu zo za African Sports na Coastal Union tumekaa na viongozi wa vilabu vyote viwili na tutaendelea kutengeneza ari ya kurudisha ari ya wanamichezo."
"Haipendezi sana kuona mwanatanga yani anafurahia timu za nje zikifanya vizuri lakini timu ambazo ziko ndani ya mkoa wa Tanga zitakuwa hazimo ndani ya moyo wake wenzetu walifanikiwaje katika maeneo mengine na sisi kwanini tushindwe ule uhasama na utani wa jadi kwaajili ya kunyanyaua mpira wa Tanga lazima uweze kurudi" alisema Rajab.
Akizungumza katibu mkuu wa Coastal Union 'Wanamangushi' kufwatia tukio hilo amesema hatua hiyo ambacho inakwenda kurudisha ari ya michezo kwa wapenda soka wote wa Tanga huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuishudia timu yao akitupa kijembe kwa mahasimu wao pale watakapokutana siku hiyo ya jumamosi.
"Tumshukuru sana mwenyekiti wa CCM kwa ajili ya kujitoa katika kuhakikisha tunaimarisha hali ya kimichezo katika mkoa wetu wa Tanga hii inaonyesha viongozi wa namna hii wanawajali wananchi na wanaijali tathnia ya michezo hili jambo alilolifanya la kujitolea shilingi millioni 30 kwaajili ya kuwekwa taa katika uwanja wetu sio jambo dogo, niwaombe mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kuishudia timu yao" alisema Rajab.
Akizungumza kwa niaba ya timu ya African Sports ' Wanakimanu manu ' Rashidi Hassan amesema kuwa mechi hiyo na mahasimu wao haitakuwa rahisi kama wanavyoichukulia akiwataka wajipange huku akiwapongeza CCM kwa hatua hiyo ambayo inazidi kuongeza chachu ya michezo kwa mkoa wa Tanga.
"Tunamshukuru sana mwenyekiti wa CCM kwa jambo hili ni huduma ambayo tulikuwa tunaisubiri kwa muda mrefu sana na tunaamini atatufanyia makubwa zaidi kikubwa wanachama wa Caoastal na African Sports waje kwa wingi waujaze uwaja wa mkwakwani hata watu wa nje wajue kama kweli Tanga kuna timu mbili mahasimu, wenzetu wa Coaastal wanaongea sana yote washamaliza ila sasa tukutane uwanjani siku ya jumamosi" alisema Rashidi
Uwanja wa CCM Mkwakwani ambao ulijengwa mwaka 1974 upo katikati ya jiji la Tanga ambapo una uwezo wa kuingiza mashabiki elfu 11 kwaajili ya kushudia michezo na matukio mbalimbali.
Post A Comment: