Na Mwandishi wetu, Dodoma

CHAMA cha wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimepata viongozi wapya ambao wataongoza chama hicho kwa miaka mitatu katika mkutano mkuu uliofanyika hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Viongozi wapya wa chama hicho, wamechaguliwa juzi katika mkutano  mkuu wa JOWUTA  ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari, mhandisi Kundo Methew.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Msajili wa vyama vya wafanyakazi nchini, Pendo Perega, Afisa Kazi mwandamizi kutoka Ofisi ya Kamishna wa kazi Makao makuu Dodoma, Honesta Ngolly, Naibu Mkurugenzi Idara ya habari ya Maelezo, Rodney Thadeus na Mkurugenzi wa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) Kenneth Simbaya .


Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo, Honesta Ngolly kutoka Ofisi ya Kamishna wa kazi Makao makuu, amemtangaza  mwandishi mwandamizi wa magazeti ya Mwananchi Communication Ltd (MCL), Mussa Juma kushinda  nafasi ya Mwenyekiti wa JOWUTA baada ya kupata kura 58 kati ya 61, mbili zikiharibika na moja ya hapana na alikuwa   mgombea pekee.

Ngolly alimtangaza  Saphia Ngalapi kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti baada ya kupata kura 42 dhidi ya Bahati Nyakiraria aliyepata kura 18, huku Suleiman Msuya akichaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu baada ya kupata kura 42 dhidi ya Mike Mande aliyepata kura 19.

Katika Uchaguzi huo, Lucy Ngowi alishinda nafasi ya Mweka hazina kwa kupata kura 49 dhidi ya Grace Mwakangare aliyepata kura 12.

Ngolly alimtangaza Said Mmanga kushinda nafasi ya naibu Katibu Mkuu baada ya nafasi hiyo wagombea kuingia katika duru ya pili, Mmanga alipata kura 33 dhidi ya kura 26 za Robinson Wangaso ambapo awali Sangito Msafiri alipatakura 9

Katika Uchaguzi huo walichaguliwa wajumbe watatu wa bodi ya udhamini ambao ni Rutta Robert alipata kura 51,Tausi Mbowe aliyepata kura 43 na Claud Gwandu kura 27.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa Juma, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) ameahidi kushirikiana na viongozi wengine na Serikali kudai maslahi bora kwa wanahabari.

Juma amesema kwa kuzingatia sheria JOWUTA itaungana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha waandishi  wanaofanyakazi kuwa na mikataba ya kazi,kuwa na bima na kuwataka waandishi nchini kujiunga na JOWUTA.

"Lakini pia kama ambavyo alishauri Msajili wa vyama tutahakikisha ndani ya muda mfupi tunakuwa na na mkakati wa kazi(Strategy plan) Ili JOWUTA iweze kuwa na sehemu ya kuanzia kufanya kazi na kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato.


Wajumbe baraza la JOWUTA na Kamati tendaji

Katika mkutano huo, kila mkoa ulichagua mjumbe mmoja wa baraza la wafanyakazi na mjumbe mmoja kila Kanda kuungana na kati ya Utendaji.

Bahati Nyakiraria alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati Utendaji kutoka Kanda ya kaskazini,Ratifa Ganzel Ganzel Kanda ya Mashariki na Grace Mwakalinga Kanda ya juu kusini.

Wengine ni Robinson Wangaso Kanda ya Ziwa, Mwajabu Hoza Kanda ya Magharibi, Editha Majura (Kanda ya Kati).

Waliochaguliwa ni baraza la wafanyakazi ni Nasra Abdalah (Dar es Salaam) Emanuel Ibrahim (Geita) Witney Joseph (Mara) Seif Mangwangi (Arusha) Rehema Cleopas (Tabora) na Msafiri Sangito (Pwani), Ashura Kazinja (Morogoro) na Asha Mwakyonde (Dodoma).

Wengine waliochaguliwa kuwa wajumbe wa baraza ni pamoja na Elizabeth Nyivambe (Mbeya), Beatha Yosam (Njombe) na Adela Madyane (Kigoma).

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya mgeni rasmi, Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya habari Maelezo, Rodney Thadeus amesema serikali itashirikiana na JOWUTA na akataka waandishi wa habari nchini kujiunga na JOWUTA Ili iwe rahisi kutatua changamoto zao.

Kwa upande wake Msajili wa vyama vya wafanyakazi Pendo Perega alipongeza JOWUTA kufanya mkutano Mkuu kwa kuzingatia sheria na taratibu na kuahidi kushirikiana na chama hicho Ili kuwasaidia wanachama wake.

Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya pia aliahidi UTPC kushirikiana na JOWUTA na kueleza tayari wameingiza JOWUTA katika mpango kazi wake kwa kuzingatia bila maslahi bora kwa waandishi hata uhuru wa habari haitakuwa na faida kubwa.


Share To:

Post A Comment: