Mkuu wa mkao wa Tanga Omari Mgumba akizungumza na wadau wa mahakama pamoja na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa wiki ya msaada wa kisheria iliyoandaliwa na mahakama kuu kanda ya Tanga.
Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Tanga Ratifa Mansoor akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya kisheria iliyofanyika katika viwanja vya Urithi Tanga leo january 22,2023.
Na Denis Chambi, Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewatahadharisha wazazi , walezi na jamii kwa ujumla wanaoendelea kumalizana kienyeji na wahalifu wa vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto akiwataka kuachana na tabia hiyo ambapo amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani pale wanapobainika.
Akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya kisheria kwa mkoa wa Tanga Mgumba amesema kuwa zipo taarifa za baadhi ya wazazi na walezi kumalizana kienyeji na wahalifu pale yanapotokea matukio ya kiukatili katika jamii badala ya kuwapeleka kwenye mikono ya sheria wanasuluhisha wenyewe hali ambayo ni kinyumr cha sheria na haki za kibinafamu.
"Tunalaani vitendo vya wazazi na walezi wanaomalizana wenyewe kwa wenyewe na wahalifu wa ukatili kwenye jamii ,kwanza hawana mamlaka hayo na ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu kisheria pamoja na katiba ya nchi suala hili ni kosa la kijinai kama jinai zingine zozote wazazi hawana mamlaka wala sheria ya kumaliza kesi zozote wenyewe kwa wenyewe hata ikitokea baba mtu kafanya kosa dhidi ya mtoto wake bado ni mkosaji na ni mhalifu kama walivyo wahalifu wengine, nitoe rai kwa wananchi kwamba waache kumalizana kesi za kijinai kwa ngazi za familiya au jamii" alisema Mgumba
"Sisi kama serikali tutaendelea kuchukua hata stahiki kwa wahalifu wote wanaotekeleza vitendo vya kikatili kwa watoto wetu na wanajamii wengine , ukatili Tanga haukubaliki na sisi tumejipanga kuendelea kuwashughulikia wananchi wote wanaotekeleza vitendo vya kiunyanyasaji hususani kwa watoto" alisema.
"Kwa mujibu wa katiba ibara ya 7(a) inaitaka mahakama kutochelewesha haki bila sababu za msingi rai yangu kwa mahakama kutekeleza takwa hili la kikatiba tuendelee kumaliza kesi zetu kwa wakati ili kupunguza malalamiko, lakini pia kuendelea kutoa haki bila kujali nafasi ya wahusika katika jamii" alisema
Kwa upande wake Mstahiki meya wa halmashauri ya jiji la Tanga Abdurahman Shillow ameipongeza mahakama kanda ya Tanga kwa namna inavyoendelea kuhudumia wananchi ikiwemo kutatua migogoro mbalimbali kwa wananchi pamoja na kuwapatia msaada wa kisheria jambo ambalo limeweza kupunguza na kuondoa kwa kiasi kikubwa malalamiko katika jamii.
"Niishukuru sana mahakama kanda ya Tanga pamoja na watendaji wake wote tunapongeza kwa sababu hii inatoa hamasa na uelewa mkubwa kwa wananchi kujua kama mahakama ipo na inahudumia jamii ambao ndio wadau wakubwa wa shughuli zote za mahakama na tunajua kama katika usuluhishi wa migogoro ndio njia muafaka kwa sababu kunakua na uwiano na maridhiano baina ya pande zote mbili tofauti wakikitumia vyema kipengele cha usuluhishi" alisema Shillow.
Akizungumza naibu msajili wa mahakama kuu Kanda ya Tanga Beda Nyaki alibainisha kuwa bado jamii ina uelewa mdogo wa maswala ya kisheria hivyo katika kuitumia vyema wiki hii ya msaada wa kisheria kwa kushirikiana na wadau wa mahakama wamejipanga kutoa elimu bure kwa wananchi kupotia njia mbalimbali juu ya maswala yanayohusu sheria ili kuongeza uelewa zaidi sambamaba na kutatua migogoro iliyopo ikiwemo ukatili.
"Tafiti zinaonyesha changamoto ya wananchi wengi wana uelewa mdogo wa maswala ya kisheria kwahiyo tupo na wadau wetu hapa ili kusaidia kuwapa wananchi elimu hasa juu ya madhara ya ukatili sote tunafahamu ukatili ni suala ambalo linatakiwa liwe na adhabu kali kwa wanaotekeleza makosa haya na pia kupata fidia stahiki kwa wahanga na hilo tunaendelea kuto elimu zaidi"
Kuelekea kuanza kwa mwaka mpya wa shughuli za mahakama kote nchini ambayo ni february mosi mahakama ya Tanga kwa kushirikiana na wafau mbalimbali wa sheria imejipanga kutoa elimu bure kwa wananchi katika wiki hii ya msaada wa kisheria kwa siku saba mfululizo hii ikilenga hasa kuongeza uelewa kwa wananchi pamoja na kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Wiki ya msaada wa kisheria kwa mwaka huu wa 2023 imebebwa na kauli mbiu isemayo 'umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu, wajibu wa mahakama na wadau.
Post A Comment: