Na John Walter-Karatu
Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Mangola Juu Kata Ya Daa
wilayani Karatu mkoani Arusha amefariki dunia baada ya
kushambuliwa na mbogo.
Tukio hilo limetokea tarehe 23 Januari mwaka huu wakati mwanamke huyo
aitwaye Katarina Ngaida akimsindikiza mtoto wake shule.
Akielezea kuhusu tukio hilo diwani wa kata ya Daa, Alex Martin
Sidawe amesema mama huyo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa
hospitalini.
Kufuatia tukio hilo diwani wa kata hiyo ameiomba serikali
kufungua shule mbili mpya ambazo zimejengwa ili kuwaondolea
adha wazazi ya kuwasindikiza watoto kwa kuwa shule ziko mbali.
Post A Comment: