Atua hiyo ya Mbunge inatokana na maombi kutoka kwa vijana hao,suala ambalo lilimlazimu Mbunge Iddi kuomba Halmashauri ya ya Msalala ikubali kutenga fedha kiasi Cha Tsh. 38,090,000 (milioni thelathini na nane na Elfu tisini) Kwa ajili ya kununua pikipiki 13 ambazo zitachochea shughuli zao za uzalishaji na kusaidia kufanyika Kwa ufanisi zaidi ili vijana hao waweze kujiinua kiuchumi.
Aidha, Mhe.Iddi Kassim Iddi amesisitiza vijana kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa Halmashauri Ili waweze Kujenga uchumi imara Kwani vijana ndio Nguvu Kazi ya Taifa.
"Tunatambua vijana ndio nguzo ya Taifa niwaombe vijana wenzangu undeni vikundi mje mchukue mikopo kama kuna changamoto inayokwamisha niambieni mimi Mbunge wenu nitawasaidia"Iddi Kassim Iddi Mbunge Jimbo la Msalala.
Aidha, amepongeza na Kutoa wito Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Ndg. Charles E.Fussi kuendelea Kutoa Pikipiki kwa vikundi vyote vya Bodaboda vya Msalala.
Pia Mbunge Iddi ameongeza adhima yake kubwa ni kuona vijana wanaimarika kiuchumu ndani ya Jimbo la Msalala .
Post A Comment: