WATOTO milioni 1.7 duniani wanaishi na virusi vya Ukimwi na kati yao watoto 160,000 ni maambukizi mapya ya mwaka 2022.
Kutokana na hali hiyoMakamu wa Rais Dk Philip Mpango leo anatarajiwa kuzindua mkakati wa kidunia wa kutokomeza Ukimwi kwa watoto ifikapo mwkaa 230.
Aidha timu ya wataalamu wa nchi 12 za Jumuiya ya Afrika wamekutana kujadili mkakati huo wa pamoja ya kupunguza watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo kwa watoto.
Hatua ya mkutano huo inatokana na mkutano wa kidunia katika mapambano ya UKIMWI, uliofanyika Agosti mwaka 2022 nchini Canada ambao kati ya maazimio yaliyofikiwa ni kuona haja timu ya wataalamu wa Afrika kukaa pamoja kuweka mkakati wa kumaliza maambukizi ya VVU kwa watoto.
Akizungumza leo Februari 1,2023 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa UN AIDS Winnie Byanyima amesema kwamba ripoti iliyotokana mwaka 2022 inaonesha watoto 96000 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo huku akifafanua nusu ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi duniani kote ni watoto.
Aidha amesema kumekuwepo na jitihada ambazo zinaendelea kuchukuliwa katika kuwalinda watoto na maambukizi hasa wakati wa mama mjazito anapojofungua na wakati wa kunyonyesha na mkakati uliopo ifikapo mwaka 2030 maambukizi kwa watoto yawe yamekwisha.
"Wadau wa sekta ya afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamekutana kwa lengo la kutafuta suluhu ya kuondoa maambukizi ya vizuri vya UKIMWI kwa watoto.Ili kuondoa maambukizi kwa watoto ifikapo 2030 tumekubaliana kuchukua hatua mbalimbali zenye lengo za kuondoa maambukizi.
"Kuondoa maambuzi kwa watoto ni jambo linalowezekana kwani Sayansi ipo na madaktari wapo hivyo ni kuwepo kwa makubaliano , hivyo tumedhamiria kuondoa tatizo na ndio maana tumekutana nchini Tanzania kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili."
Alipoulizwa ni jinsi gani ambavyo wameweka mkakati wa kumlinda mtoto wa kike(msichana) Byanyima amesema zipo hatua mbalimbali zinachukukuliwa kumlinda mtoto wa kike ikiwemo kutoa elimu ya kujitambua na kujilinda huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwamba njia nzuri inayoweza kumuepusha msichana kwenye kupata maambukizi ni kumpeleka shuleni kwani tafiti zinaonesha inapunguza kwa asilimia 15.
Awali wakati wakizungumza kwenye majadiliano mbalimbali kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Makamu wa Rais wa Zimbabwe Constantine Chiwenge amesema kwenye nchi yao watu milioni 1.1 wanaishi na virusi vya UKIMWI na wengi wao ni watoto.
Amesema wameendelea na hatua mbalimbali za kuhakikisha wanakabiliana kukomesha mamabukizi ya ugonjwa huo na sasa wamepunguza kwa asilimia 30 lakini akaeleza baada ya kuona hali hiyo kueleza waliamua kuweka mikakati madhubuti kupunguza maambukizi kwa kushirikisha wadau na wananchi kwa ujumla.
"Kutokana na changamoto iliyopo tuliamua kukaa na kuweka mkakati madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na vizuri vya UKIMWI na miongoni mwa mkakati tuliyochukua ni kumlinda mama mjazito wakati wa kujifungua pamoja na kutoa elimu kwa wasichana.Pia kuwahimiza wanaume na vijana ambao walikuwa nyuma kwenye mapambano ili nao washiriki kikamilifu."
Kwa upande wake Mwakilishi wa vijana wanaoishi na virusi vya UKIMWI Pudensiana Mbwiliza amesema kuwa ili kukabiliana na maambukizi hayo ni vema vijana wa kiume wasiachwe nyuma kwani ndio wazazi wa kesho huku akitumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa huo lakini pia kuondoa unyanyapaa wa kijinsia katika mapambano ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Post A Comment: