John Walter-Manyara.
Kampuni ya Mati Super Brands limited iliyoko mkoani Manyara imeshiriki katika kampeni ya kupanda miti 5000 kwenye eneo la Ziwa Babati ili kurejesha uoto wa asili na kulinda ziwa Babati lisipotee .
Akizungumza wakati wa zoezi la Upandaji Miti ,Mkurugenzi wa Kampuni hiyo David Mulolkozi amesema kuwa wameamua kungana na wadau mbali mbali wa mazingira ikiwemo uongozi wa Miss Jungle Tanzania na Serikali ya mkoa ili kuwezesha zoezi la upandaji miti pembezoni mwa ziwa Babati.
Mulokozi amesema kuwa jamii inapaswa kuunga mkono kampeni hiyo itakayohakikisha kuwa ziwa hilo halipotei kutokana na shughuli za kilimo pembezoni mwa ziwa hilo suala linalohitaji juhudi za pamoja za serikali na wadau.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amepongeza juhudi za wadau wa Maendeleo ikiwemo kampuni ya Mati Superbrands na wadau wengine kwenye kuunga mkono kampeni zinazofanywa na serikali za kupanda miti ili kulinda mazingira.
Kwa upande wake Miss Jungle 2022 Doreen Gibson ameeleza kufurahishwa na zoezi la upandaji miti ambalo limeshirikisha mamia ya wananchi pamoja na viongozi wa serikali .
Post A Comment: