Na Joel Maduka Geita.
Waumini mbali mbali wa Dini ya Waadventista Wasabato Nchini wametakiwa kutambua majira na nyakati kwa kutenda mambo yaliyo mema ikiwa ni pamoja na kuwavuta watu kumtambua Mungu na kuachana na vitendo viovu ambavyo vimeonekana kuendelea kuugubika Mkoa wa Geita.
Hayo yamesemwa na Askofu wa Jimbo la Nyanza ukanda wa Dhahabu wa Kanisa la waadventista wasabato ,Enoch Sando ,wakati akizungumza na waumini wa kanisa hilo kwenye uzinduzi wa Mtaa wa Nyankumbu uliopo Mjini Geita.
Amesema ni vyema kwa waumini wa dhehebu hilo wakatumia muda wao mwingi kufanya tafakari ya Mungu ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vya uovu ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watu ambao bado awajamjua Bwana Yesu Kristu.
Post A Comment: