.

 Na Farida Mangube.


Serikali wilayani Morogoro imesema imeenza kuchua hatua za awali za kuwahifadhi na kuwapatia chakula waathilika wa mafuriko yaliotokea January 13.


Akizungumza kwa njia ya simu Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Ally Machela  alisema msaada ulioanza kutolewa ni pamoja na mchele, Unga wa mahindi, maharage na dagaa huku wakiendea  kufanya tathimini ya athari zilizotokea kwa watu.

Hatua walizozichukua ni kuwapelekea chakula na nakuona maeneo gani watakaa lakini alisema wengi wanakaa kwa ndugu na jamaa huku wengine wakilejea kwenye  nyumba zao kufanya usafi na ulinzi zaidi.

" maeneo ya kata ya Tungi tulipeleka chakula kwa familia 12, na kata za kihonda na Lukobe walipeleka mifuko 35 ya chakula na sasa." Alisema Mkurugenzi.


Alisema karibu watu wote walioathirika kwa kushirkiana na viongozi wa kata za kihonda, Tungi  na Lukobe ambao walikuwa wakipita nyumba kwa nyumba kuhakikisha kila familia walau inapata unga kilo 20, mafuta ya kula,dagaa maharage na chumvi.

Aidha alisema Halmashauri ya manispaa morogoro, Wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura), Mradi wa ujezi wa Reli ya kisasa(SGR), na Wakala wa barabara Tanzania(Tanroads) imeundwa kamati ambayo inatengeneza ripoti ya kitaalamu ili kufahamu hali halisi ya namna watu walioathirika.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Morogoo Albert Msando  alisema maeneo ya Kihonda na Mkundi ambayo yanalalamikiwa kama mkondo wa maji na wananchi imeudwa kamati maalumu ya kuzunguka maeneo hayo yote ili kuleta nini kifanyike na kwamba inafanyiwa kazi.

Nae Mwenyekiti wa mtaa wa Kihonda B Hamis Mselemo alisema katika mtaa wake  kaya 78 zimeathirika na mafuriko hayo ambapokuna nyu7ma zimeezuliwa paa na kubomoka kabisa na kusombwa na maji.

Alisema tayari wameanza kupokea msaada kutoka serikalini na wameanza kuwapatia chakula wale wote wanaotakiwa kupewa, huku akieleza kuwa wengi wa walipta kadhia hiyo wamehifadhiwa kwa majirani, na ndugu.

Kaimu kamanda Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Morogoro    Mkaguzi Emmanuel Ochieng alisema mpaka sasa watu waliookolewa ni 59 ambapo watoto 39 na watu wazima 20 na kwamba wote wapo katika hali nzuri.

Ochieng alisema Zimamoto ineandelea na kuangalia wananchi wa maeneo yote yaliyoathirika na maji ya mvua huku akiwataka kutoa taarifa pindi wanapoona kuna madhara


Share To:

Post A Comment: