Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  Wilaya ya Iringa Mjini Shedrack Masanika akigawa mahitaji kwa Watoto yatima ya kituo cha Huruma Center
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  Wilaya ya Iringa Mjini Shedrack Masanika akigawa mahitaji kwa Watoto yatima ya kituo cha Huruma Center

Na Fredy Mgunda, Iringa.


JUMUIYA ya wazazi wa Chama Cha mapinduzi CCM Wilaya ya Iringa mjini imekabidhi msaada wa Vitu mbalimbali Kwa ajili ya mahitaji Kwa watoto wanaolelewa katika kituo malezi cha Huruma  (Huruma Center) ikiwa ni sehemu ya maadhimishonya miaka 46 ya matcha hicho Tawala nchini.

Kwa Mujibu wa Kamati ya maandalizi ya miongoni mwa mahitaji hayo ni pamoja na Unga wa Sembe kilo 100, Katoni za Sukari, chumvi sukari na mahitaji mengine Kwa ajili ya watoto katika kituo hicho kilichopo mtaa wa Kigamboni Kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  Wilaya ya Iringa Mjini Shedrack Masanika wakati wa Hafla yakukabidhi msaada huo alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi CCM iliyojielekeza katika kuboresha malezi ya watoto wakiwemo wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji Ili kuwajengea msingi Bora wa maisha ya baadaye.

Masanika Alisema kitendo hicho Cha kuwajali watoto wote pasipo kuwabagua ni jukumu la Jumuiya ya Wazazi hivyo aliwataka Wenyeviti wa Jumuiya hiyo ngazi ya mitaa na Kata Wilayani humo kuhakikisha wanaendelea utamaduni wa kuwatembelea na kuchangia Vitu mahitaji katika vituo vya malezi pamoja na  kuwahamasisha Wananchi na Watu wote kujitokeza kuwafariji na watoto Kwa kushiriki nao katika matukio ya furaha ili kujua mahitaji Yao na kuwasaidia Kwa kushirikiana na walezi wa vituo hivyo.

Mwenyekiti huyo alisema pamoja na msaada huo Jumuiya hiyo inapinga vikali vitendo vya Ukatili ikiwemo ubakaji na Ulawiti dhidi ya watoto na kusisitiza Kuwa Kupitia Jumuiya hiyo watahakikisha wanaisimamia Serikali na vyombo vya Dola kuona hatua za kisheria za haraka zinachukuliwa haraka Kwa watakaobainika kujihusisha Kwa namna yote na vitendo hiyo Kwa lengo la kukomesha ukatili huo.

Kwa upande wake Mjumbe mkutano mkuu wazazi anayewakilisha Wazazi Joseph Nzala Ryata aliyeshiriki katika Hafla hiyo alisema kitendo Cha Jumuiya hiyo kupeleka msaada huo, ni ishara ya wazi ya kuunga mkono Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita iliyo mstari wa mbele katika kuhakikisha Ulinzi na ustawinwa mtoto unaimarika Kwa manufaa ya Taifa na Leo na Kesho.

Ryata alisema Rais Samia Suluhu Hassan anakerwa na vitendo vya Ukatili hasa dhidi ya watoto vinavyoendelea katika maeneo mbalimbali nchini Hususani Wilayani Iringa hivyo ni wajibu wa Kila mmoja kushiriki kikamilifu Kwa vitendo katika kukomesha vitendo hivyo vya Ukatili.

Alisema katika Ilani ya Chama Cha mapinduzi suala la mlezi limeelekezwa kikamilifu hivyo suala la Ulinzi na Usalama siyonla Jeshi la Polisi pekee Bali ni la Kila mmoja hivyo aliitaka jamii kurejea katika misingi ya malezi ikiwemo kuimarisha upendo, huruma na utamaduni kwani Agenda ya malezi ni Agenda ya nchi nzima ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa kutuo Cha Huruma Mchungaji Joyce Ngandango pamoja na kukushukuru Jumuiya hiyo Kwa kuwakumbuka watoto wa Huruma Center alisema ni muhimu wadau mbalimbali wakaiga mfano huo kwani watoto wanafarijika kuona Watu mbalimbali wanawakumbuka Kwa kuwatembelea na kuwapatia mahitaji.

Mchungaji Ngandango alisema kituo hicho kinalewa watoto wa aina mbalimbali wakiwemo Yatima, waliotelekezwa na wazazi wao pamoja na waliokimbia manynyaso na ukatili katika jamii, wazazi ama walezi wao.

Hata hivyo alitoa Wito Kwa Wanandoa kuzilinda Ndoa zao Kwa kuimarisha upendo utakaosaidia kukomesha migogoro ya ndoa na Mahusiano aliyoitaja kuwa ni miongoni mwasababu kuu za ongezeko la watoto wanaonyanyasika na kukimbilia katika vituo hivyo vya malezi huku wengine wakisalia mitaani na kujiingiza katika vitendo vya Uhalifu na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM Wilayani Iringa imeendelea kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo hatua hiyo ya kutoka misaada Kwa Vituo vya malezi ya watoto ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Miaka 46 ya Kuzaliwa Kwa CCM ambapo Mkoa wa Iringa utafanya maadhimisho hayo Januari 28 katika Wilaya ya Mufindi.







  

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: