Na Janeth Raphael - Mwanga kilimanjaro
Halmashauri ya Wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro imetoa jumla mikopo146,916,000/ kwa vikundi 12 kati yake vikundi vya wanawake saba na vikundi vya vijana vinne(4 ) na kikundi kimmoja cha mtu wenye ulemavu wa viungo.
Akizungumza wakati akikabidhi mikopo hiyo leo Desemba 31,2022 mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo amesema halmashauri ya wilaya Mwanga ni miongoni mwa halmashauri inayofanya vizuri katika utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Tadayo amesema mikopo hiyo ipo kisheria na kwamba lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan nikuhakikisha vikundi vyote vilivyokidhi vigezo vinapewa ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdalah Mwaipaya amesema mikopo hiyo siyo zawadi na walengwa wahakikishe wanapeleka mikopo hiyo kwenye miradi iliyokusudiwq kwani lengo la Serikali ni kuona vikindi hivyo vinakuwa endelevu
Awali akitoa taarifa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mwanga Mwajuma Abas Nasombe amesema katika bajeti ya 2022/2023 halmashauri ilikadiriwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi million 213 kutoka kwenye bajeti ya asilimia 10 ya mapato halisi ya ndani, mpaka sasa tayar mikopo wenye thamani m.246
Mbunge wa jimbo la.Mwanga advocate Joseph Tadayo akizungumza katia hafla hiyo ya kukabidhi mikopo hiyo
Post A Comment: