WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema nchi ina ‘stock’ ya vitendanishi vya kupima malaria (MRDT) ambavyo havijamaliza muda wake.
Ummy, ameyasema hayo leo kufuatia video ya watumishi wawili kada ya afya kusambaza mtandaoni ikionyesha watumishi hao wakibishana kuhusu vipimo vya Malaria (MRDT)
Muuguzi wa kike akimlazimisha kijana wa mahabara kutumia vipimo hivyo kwa mjamzito na kijana huyo akigoma kutumia kwa kile alichodai kuwa vime expire ( kuisha muda wake).
Kufuatia hali hiyo, Ummy aliagiza Mamlaka husika kufuatialia suala hilo na kuchukua hatua huku akidai kuwa hakuna vitendanishi vya kupima malaria vilivyoisha muda wake.
Aidha, baada ya kauli hiyo ya Waziri Ummy, Halmashauri ya Wilaya ya Uyui imetangaza kuwasimamisha kazi watumishi hao wawili wa kada ya afya kutoka halmashauri hiyo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uyui, Dk Kija Maige katika taarifa yake imesema watumishi hao wameonekana wakizozana kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuleta taaruki kwa jamii.
Maige ameseme, amewasimamisha kazi watumishi hao wote wawili ili kupisha uchunguzi kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya utumishi wa umma ya mwaka 2003.
Aidha, amesema uchunguzi huo utashirikisha Mabaraza ya kitaaluma ambayo ni baraza la wauguzi Tanzania na baraza la wataalamu wa Maabara Tanzania kwa hatua zaidi baada ya kukamilika uchunguzi.
Post A Comment: