Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Morogoro ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Albert Msando ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo inalazimika kuwakamata watu 12 waliovamia katika eneo la mwekezaji na kuharibu mazao na vitu mbalimbali ikiwemo kung'oa zao la.katani
Kitendo cha uvamizi wa wananchi hao katika eneo Hilo Kimetafsiriwa kama uvunjifu wa amani kwani tayar mwekezaji huyo alishatoa ekari 4,500 kati ya ekari elfu kumi na Mia sita anazomiliki kihalali na kulitoa Kwa serikali ili kupanga shughuli mbali mbali ikiwemo makazi lakini bado wameendelea kuvamiwa eneo lilolobaki na kuanzia kulima
DC Msando alisema siku za hivi karibuni mkuu wa mkoa Morogoro Fatma Mwassa alifika katika eneo Hilo na kuwataka wananchi kuacha kufanya shughuli zozote na kusubr zoezi la uhakiki lakini siku chache badae watu wengine wamevamia shamba la mwekezaji na kufanya uharibifu nje ya eneo alilotoa serikalini kisha kugawana Kwa ajili ya viwanja na Kilimo kinyume na utaratibu.
Post A Comment: