Na Joel Maduka..Geita 


Kamati ya Siasa wilaya ya Geita Mkoani Geita imeuagiza Uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Salagulwa kata ya Nyamwilolerwa halmashauri ya wilaya ya Geita kuhakikisha wanalipa fidia wananchi waliotoa maeneo yao kwa ajili ya kujenga shule sekondari kama Fidia kwa wananchi hao ambao waliingia makubaliano na Serikali ya kijiji.



Akitoa Maagizo hayo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Barnabas Mapande mara baada ya kutembelea na kukagua shule ya sekondari Salagurwa akiongozana na Kamati hiyo ya siasa katika kukagua miradi mbalimbali katika Jimbo la Busanda mapande amemtaka Mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na Afisa Mtendaji wa kijiji kulipa fidia wananchi hao.




Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Salagurwa Peter Joseph akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba sita vya Madarasa mbele ya Kamati ya siasa  amesema kiasi cha fedha shilingi Milioni 126 zilipokelewa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambao umekuwa ni kikwazo kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu hali ambayo wameishukuru serikali kwa kutenga fedha hizo.


Taitus Kabua na Wilson Shimo ni wajumbe wa halmashauri ya siasa ya wilaya ya Geita wamempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili kujenga vyumba vya Madarasa lengo likiwa ni kupunguza changamoto ya umbali kwa wanafunzi katika halmashauri ya wilaya ya Geita.










Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: