Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Tanga wakati akitoa tamko la kumpongeza na kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt Samia Suluhu.


Na Oscar Assenga, TANGA



CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM) kimempongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimariisha demokrasia nchini huku wakitoa wito kwa wana CCM Mkoa huo kujielekeza katika kufanya siasa zenye hoja,tija na majawabu kwa watanzania wa rika zote na ambaye atakwenda kinyume chake chama kitahangaika naye

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman wakati akizungumza na waandishi wa habari akitoa tamko la wana CCM Mkoa wa Tanga la kumpongeza na kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha na kuishaurisha demokrasi Nchini.

Ambapo alisema kufuatia Rais Samia kuridhia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ni vyema kila chama cha siasa kuheshimu taratibu na sheria zilizopo ili kufanya siasa zenye utashi na ustawi wa maendeleo huku akitaka vyama vya siasa kutumia nafasi walioipata kuheshimu taratibu zilizopo ili kufanya siasa za kistaarabu.

"Ndugu zangu waandishi nimewaita leo hii ili kuongea na wana CCM na watanzania kwa ujumla kuongea juu ya mambo makubwa mawili ambayo mwenyekiti wa ccm Taifa na Rais dkt Samia Suluhu Hassan kayapanga kwa upendo mkubwa kwa watanzania na vyama vyote nchini moja kukubali maridhiano ya mazungumzo baina ya serikali ya ccm chama cha mapinduzi na vyama vingine vya siasa vipavyo 18,"

Alisema kwamba baada ya kuruhusiwa kufanyika kwa mikutano ya siasa hawata mvumilia au kuona mwanasiasa yeyote ambaye atakuwa na nia ovu ndani ya ccm na nje ya ccm ya kuvuruga mikutano ya vyama vya siasa ambalo ni tamko lililoruhusiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Kuridhia na kukubali yeye binafsi na chama cha mapinduzi juu ya kuruhusu kazi ya kuimarisha siasa ya vyama vyote nchini kuendelea kufanya siasa bila upendeleo kwa kuruhusu mikitano ya hadhara hivi karibuni alipokutana na vyama vyote hivyo kama Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na kwaniaba ya wana CCM na wananchi wote wa Mkoa wa Tanga tunatoa pongezi nyingi kwa hatua hii ambayo imeonyesha kuwa Rais ni mtu mwenye hofu ya Mungu na amejua na kuelewa kwa busara za hali ya juu kuliongoza Taifa letu na wananchi wake, "Alisema Mwenyekiti Rajab.


Mwenyekiti Rajab alisema mchakato huo ulianza kwa mazugumzo ambayo yalipelekea kuunda kikosi kazi kitakachofanya kazi kwa weledi na ustadi zaidi ili kutoa maoni na ushauri namna ya kufanya siasa baina ya vyama vyote nchini ambapo kazi hiyo haikuwa rahisi kama wanavyofikiria.

Alisema jambo hilo lilihitaji uongozi makini na wenye busara za kiungozi ili kupokea na kufanya maamuzi juu ya kuridhia kuanza siasa kwa usawa wa vyama vyote hivyo kutokana na hilo wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Maono ya Mwenyekiti wetu wa ccm na Rais yamejikita katika mawazo ya (4R) maridhiano na ustahamilivu katika mabadiliko ya kujenga umoja na mshikamano baina yetu sisi kama watanzania na wanaccm tunapaswa kumpa ushirikiano mkubwa kufanya jambo hili kuwa na ukweli wa wazi ili kila mmoja wetu afaidi matunda ya mawazo yake, "alisisitiza Rajab.

"Kwa muktaza huo wanaccm na wananchi wa Mkoa mzima wa Tanga nimesimama mbele yenu kuelezea furafa yetu katika jambo hili muhimu lenye tija kwa maendeleo ya watanzania wote wapenda amani pia tunaelekeza mawazo yetu na nguvu zetu katika kulisimamia na kuliishi tanko hili ambalo ni dira maendeleo ya siasa, "

Aidha amewataka viongozi na watendaji wa serikali kusimamia maelekezo ya Rais kwa vitemdo bila kusahau kuimarisha ulinzi na usalama kwa kila mtanzania.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Salim Mohamed Ratco wakati huu serikali imefungua pazia la mikutano ya hadhara ni vyema vyama vyote vizingatie sheria na kanuni zinavyoeleza wakati wakitekeleza wajibu wao.

"Kila kitu kina mipaka yake ukikengeuka ukasema mambo yasiyofaa sheria itachukua mkondo wake ni vyema kila mwanasiasa akafuata taratibu sheria na kanuni za mikutano zinavyotaka, "alisema Ratco.

Alisema jambo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la kuruhusu mikutano ya hadhara lengo ni kupana wigo wa siasa nchini ikiwemo kurekebishana, kutoa maoni na kushauriana ili isaidie kuchochea maendeleo.


Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo


Share To:

Post A Comment: