Na Denis Chambi, Tanga.

CHAMA cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na serikali kupitia watendaji wake kimesema kuwa kimejipanga kuhakikisha kuwa kinamaliza na kutokomeza kabisa migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambayo imekuwa ikileta athari mbalimbali kwa wananchi. 

Akieleza mikakati kwa miaka mitano ijayo mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Rajab Abdurahmani wakati alipokutana na sekretarieti yake amesema kuwa kumekuwa na migogoro mingi ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu hivyo kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa watakaa kushirikiana kwa pamoja kutafuta suluhisho la kuondoa migogoro hiyo.

 "Nilivyopokea kijiti hiki cha uongozi kulikuwa na mogogoro mingi ya ardhi hususani katika wilaya za Kilindi , Handeni na baadhi ya maendeo mengine lengo letu kama chama cha mapinduzi ni kukaa na serikali , kamati ya ulinzi na usalama mkoa tukishirikiana kwa pamoja kutafuta namna bora na iliyo nzuri zaidi kuweza kuiondoa migogoro hii au kuipunguza kwa kiasi kikubwa" alisema Rajab. 

"Katika uongozi wangu kwa miaka mitano nikishirikiana na viongozi wote tunataka CCM iendelee kuwa kimbilio la wananchi wote wanaoishi mkoa wetu wa Tanga kila mmoja atapata haki yake hakuna atakaye onewa , tutaendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ipasavyo tena kwa vitendo " aliongeza Aidha Rajab amesema kuwa atahakikisha chama hicho kinaendelea kujiimarisha kisasa na kiuchumi ambapo wamejipanga kusimamia na kuongeza vyanzo vyake vya mapato ili waweze kutekeleza mipango yao kwa vitendo. .

 " Lazima kukiimarisha chama chetu kisasa na kiuchumi , hatuweze kufanya siasa ikiwa hatuna uchumi imara ndani ya chama chetu ndani ya mkoa wa Tanga, lazima tuweze kuzalisha vyanzo vya mapato ndani ya mkoa wetu lazima tuumize vichwa kwanza kusimamia rasilimali zilizopo na kutafuta vyanzo vingine tena vikubwa kwa chama na jumuiya zake " alisema .

Hata hivyo mwenyekiti huyo amewatahadharisha wanachama wa chama hicho wenye nia ovu ya kutaka kuleta migogoro ndani ndani na nje ya chama badala yake amewataka kuheshimu katiba, miongozo ,kanuni na taratibu zote zinazowaongoza. 

"Ni wajibu wa kila mwanachama kuiheshimu katiba ,miongozo kanuni na taratibu za chama chetu , sitaraji kuiona migogoro ndani ya chama chetu isiyokuwa ya lazima, hatutarajii kuona mwana CCM ndani ya mkoa wa Tanga anakuwa kipaumbele au kinara kuvunja taratibu za chama chetu tena kwa maksudi kabisa" alisema 

Sambamba na hayo Rajabu ameshangazwa na idadi ndogo ya zoezi la uandikishaji wa wanafunzi kwa mwaka huu wa masomo hivyo kuahidi mara baada ya kukutana na kamati ya siasa ya chama hicho kwenda kuwabana wazazi na walezi wote ambao hawajawapeleka watoto wa shuleni. 

"Suala la unadikishaji kwa mkoa wa Tanga sisi wenyewe kama chama lazma tusikitike kwa sababu madarasa yapo serikali imejenga kila kona , madarasa na madawati yapo lakini watoto hawajaenda kuandikishwa tutabanabana ili kila anayepaswa kutimiza wajibu wake anawajibika"alisisitiza.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  'CCM' mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman (katikati) akizungumza na watumishi wa sekretarieti ya chama hicho  katika ofisi yake  January 17 , 2023 wakati aliporipoti rasmi kuanza majukumu yake ya kukitumikia chama .


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  'CCM' mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman akisistiza jambo wakati akizungumza na watumishi waliopo katika ofisi yake January 17, 2023 .
Share To:

Post A Comment: