CHAMA cha mapinduzi mkoa wa Tanga kimempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Smia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho taifa kufwatia agizo uamuzi aliouchukuwa hivi katibuni wa kuondo zuio la mikutano ya vyama vya siasa hapa nchini wakisema kuwa maamuzi hayo ni ya busara na yamelenga kuinarisha demokrasia huku akiwataka viongozi wa vyama vingine na watanzania kwa ujumla kuendelea kudumisha amani na utulivu nyakati zote kwa maslahi mapana ya Tanzania.
Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman katika mkutano wake na vyombo mbalimbali vya habari ambapo amesema kuwa kila mmoja anatakiwa kutanguliza mbele maslahi ya Taifa kwa kuhakikisha kuwa amani umoja na mshuikamano vinadumishwa nyakati zote
"Kwa upendo mkubwa rais wetu amekubali maridhiano na mazungumzo baina ya serikali na vyama vingine vya siasa hapa nchini , kuridhia na kukubali kuruhusu kazi ya kuimarisha siasa kwa vyama vyote nchini bila upendeleo mambo ambayo ni muhimu sana katika taifa letu , kwa niaba ya chama cha mapinduzi na wananchi wote wa mkoa wa Tanga tunatoa pongezi nyingi sana kwa hatua hii kuonyesha rais wetu ni mtu mwenye hofu ya Mungu na muelewa juu ya kuongoza wananchi wote wa Tanzania" alisema Abdurahman.
"Maono ya Rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania yamejikita katika mawazo makubwa muhimu sana maridhiano na ustahimilivu wa kujenga ushirikiano baina yetu sisi kama watanzania tunapaswa kumpa ushrikiano mkubwa ili kufanya kila mmoja wetu afaidi matunda ya mawazo ya rais wetu na wapenda amani miongoni mwetu hivyo tukubali kukosao na kukosolewa ili tuweze kujenga maendeleo ya kila mmoja "
Aidha amewataka viongozi wa serikali kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha amani utulivu na umoja vinaendelea kudumishwa nyakati zote itakapofanyika mikutano ya kisasa baina ya watanzania.
"Katika kufanya siasa yenye hioja na tija na majawabu kwa watanzania wote nawaomba sana viongozi na watendaji wa serikali kusimamia suala hili kwa viendo bila kusahau kuimarisha ulinzi na usalama kwa vyama na kila mtanzania kwa rika zote, tunaendelea kutoa ahadi yetu kwake kuwa ccm tutaendelea kutekeleza maagizo yake yote ili kufikia malengo mahususi yaliyokusudiwa ili kuwaletea maendeleo yenye tija watanzania wote"
Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa chama chama hicho hakitamvumilia mwanachama wake au mwanasisasa yeyote atakayekuwa na nia ovu ya kutaka kuvuruga amani ya nchi kupitia majukwaa ya kisiasa na kuahidi kumchukulia hatua kali za kisheria kwa maslahi mapana ya Tanzania
"Chama chetu hakitamvumilia au kuona mwanasisasa yeyote ambaye atakuwa na nia ovu ndani na nje ya CCM kuvuruga jambo hili , CCM itahangaika naye ili kupata heshima inayostahili kwa mheshimiwa Rais wetu, niwaombe sana wanasiasa na watanzania kufanya jambo hili la mfano sana kukubali kukosolewa na kukosoa kwa mslahi ya wananchi wote" alisema Rajabu.
Awali akizungumza mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa Mohammed Salimu 'RATCO ' amesema kuwa hatua hiyo ya Rais Samia Suluhu Hassan itatoa fursa kwa chama chake kueleza na kunadi maendeleo kwa wananchi yaliyoletwa na kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa na serikali
Kupitia mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman kimetangaza nia yake ya kuanza rasmi mikutano hadhara ifikiapo February 15, 2023.
Post A Comment: