Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi George Kavenuke akiongea na Halmashauri kuu ya CCM kata ya Mapanda namna gani diwani wa kata hiyo amekuwa akijituma kufanya kazi la kuleta maendeleo ya wananchi kata hiyo.
Diwani wa kata ya Mapanda Obadia Kalenga akieleza namna gani anavyotekeleza ila ya CCM kata ya Mapanda
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kata ya Mapanda

Na Fredy Mgunda Iringa.


CHAMA cha mapinduzi wilaya ya Mufindi (CCM) kimempongeza Diwani wa kata ya Mapanda kwa kubuni, kusimamia na kuanzisha miradi ya kimaendeleo ambayo inachochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa kata hiyo.
Akizungumza katika kikako cha Halmashauri kuu ya kata ya Mapanda,mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi (CCM) George Kavenuke alisema kuwa Wananchi wa kata hiyo wamekuwa na maendeleo yanayoenda kwa kasi kubwa kutokana na mchango mkubwa wa diwani wa kata hiyo Obadia Kalenga.

Kavenuke alisema kuwa diwani wa kata hiyo amekuwa mpambanaji kwa kuhakikisha wananchi wa kata ya Mapanda wanapata maendeleo na kukuza uchumi wao kwa kuboresha miundombini,maji,elimu na kilimo ambavyo ndio uti wa mgogo wa maendeleo ya wananchi.

Alisema kuwa kata ya Mapanda imebadilika kwa kipindi kifupi kutokana na mshikamano wa serikali, Chama na diwani ambao kwa pamoja wanachangia maendeleo ya wananchi kwa kukuza uchumi.

Kavenuke aliwataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kukuza uchumi na kufanya maendeleo ya wananchi ambao ndio wamekuwa wakiiweka serikali madarakani.

Alisema kuwa wanachama wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kujibu hoja za wapinzani kwa hoja sio kwa ugomvi hivyo chama kimeanda mkakati maalum wa kutoa elimu kwa wanachama wote kupitia idara ya uenezi.

Kavenuke alimazia kwa kusema kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa wilaya ya Mufindi atafanya ziara kila kata na Kijiji kutoa elimu ya namna ya kuyasemea mambo mazuri ambayo yanafanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mapanda Obadia Kalenga alisema kuwa kwa mwaka huu wa fedha wamepata kilometa 31 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Ukami hadi Mapanda kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa wananchi.

Kalenga alisema kuwa kukumilika kwa ukarabati wa barabara hiyo Kutachochea kwa kiasi kikubwa uchumi wa wananchi wa kata ya Mapanda na wilaya kwa ujumla kutokana shughuli za kimaendeleo zinazofanywa katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa Wananchi wa kata ya Mapanda wamekuwa wakijituma kufanya kazi za kimaendeleo jambo ambalo linasaidia kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa kata hiyo.

Kalenga alimazia kwa kusema kuwa bado kata ya Mapanda kunachangamoto ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi ili kuwasaidia wananchi kufanya shughuli za kimaendeleo bila bughuza yoyote ile.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: