Ferdinand Shayo ,Arusha
Wanafunzi walioshinda tuzo 3 katika mashindano ya Ujasiriamali yaliyofanyika Jijiji Lagos nchini Nigeria wamerejea nchini na kupokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na mamia ya wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari ya Arusha Science wakiongozana na Maafisa wa Shirika la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ambao walishiriki kuratibu mashindano hayo.
Afisa Mafunzo na Ushauri kutoka shirika la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Evelyne Kaijage aliyeambatana na wanafunzi hao huko nchini Nigeria amesema kuwa licha ya ushindani mkubwa waliokutana nao bado wanafunzi wa Kitanzania wameweza kuibuka na kuchukua tuzo tatu moja ikiwa ni ya Mkurugezi bora wa kampuni na pia kampuni bora ya ujasiriamali ya Kibega iliyobuniwa na Wanafunzi hao.
"Tunamshukuru Mungu tuzo ziliandaliwa na shirika Juniour Achievement Africa na tumerejea salama na tumerudi na ushindi ambao utatoa chachu kwa wanafunzi wa kitanzani kuendeleza bunifu zao ambazo zitatua changamoto katika jamii lakini pi kusaidia kutengeneza ajira " Alisema Avelyn
Akizungumza kwa niaba ya Washindi hao ,Mshindi wa Tuzo ya Mkurugenzi bora wa kampuni ya Kibega Koko Georgies ameeleza furaha yake baada ya kushinda ambapo ameipongeza shule yao ya Arusha science ,uongozi wa shirika la The Foundation For Tomorrow pamoja na .
Afisa elimu Mkoa wa Arusha Abel Ntupwa amepongeza juhudi za shule ya Arusha Science kwa kuwa kinara katika masomo ya sayansi pamoja na kuhimiza ubunifu kwa wanafunzi ambao umepelekea shule hiyo kupata tuzo za kitaifa na kimataifa.
Mkurugenzi wa Shule ya Arusha Science Profesa Nuhu Hatibu amesema amesema kuwa tuzo hizo zitakua chachu kwa wanafunzi na walimu kuendelea kutilia mkazo masuala ya sayansi na ubunifu.
Post A Comment: