Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akikabidhi leseni na vyeti kwa wazalishaji wa bidhaa nchini katika wa hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba 2022. Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akikabidhi leseni na vyeti kwa wazalishaji wa bidhaa nchini katika wa hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba 2022. Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika wa hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba 2022.Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Lazaro Msasalaga akizungumza katika wa hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba 2022. Baadhi ya wazalishaji wa bidhaa wakiwa katika wa hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba 2022.

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limekabidhi leseni 246 kwa wazalishaji wa bidhaa nchini na vyeti vya ubora wa mifumo (system certification) vilivyotolewa ni vitatu, huku leseni zilizoongezewa bidhaa (Licence extension) ni 35.

Ameyasema hayo leo Desemba 8,2022 Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya wakati wa hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba 2022.

Aidha amesema leseni na vyeti 128 ambayo ni sawa na asilimia 52 vilitolewa kwa wajasiriamali wadogo. Vyeti na leseni hizo ni za bidhaa za vyakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, vilainishi, vitakasa mikono, vifaa vya umeme, vifaa vya makenika, magodoro, vibebeo pamoja na vifungashio.

"Leseni na vyeti vilivyotolewa leo vitazisaidia bidhaa zilizothibitishwa kuongeza imani kwa umma juu ya ubora wa bidhaa iliyothibitishwa, zitakubalika sokoni, zitapata faida ya kiushindani (competitive advantage) na kuingia na kuuzwa katika soko la la Afrika Mashariki pasipo kufanyiwa vipimo". Amesema Dkt.Ngenya.

Hata hivyo amesema kwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili mpaka Septemba 2022 wamekwisha sajili majengo 5,228 ya biashara na ya kuhifadhia bidhaa za vyakula na vipodozi na katika kipindi hicho wameweza kusajili bidhaa 906 za vyakula na vipodozi

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: